Unknown Unknown Author
Title: HATIMAE WAGOMBEA UBUNGE MTAMA WAMALIZA TOFAUTI ZAO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na.Ahmad Mmow, Lindi. Wagombea wa ubunge katika jimbo la Mtama, wilaya ya Lindi vijijini, kutoka katika vyama vilivyopo kwenye Umoja wa Kat...
Na.Ahmad Mmow, Lindi.
Wagombea wa ubunge katika jimbo la Mtama, wilaya ya Lindi vijijini, kutoka katika vyama vilivyopo kwenye Umoja wa Katiba ya Wananchi(UKAWA), Isihaka Mchinjita(CUF) na Seleman Methew(CHADEMA) wamemaliza tofauti zao zilizotokana na mgogoro wa kugombea jimbo hilo.
UKAWA
Mgogoro ambao ulianza kuwagawa wafuasi wa wagombea hao kiasi cha pande hizo kutuhumiana kutumiwa na Chama Cha Mapinduzi(CCM).

Wakizungumza baada ya kikao kirefu cha ndani kilichofanyika katika kijiji cha Kiwalala kwenye ukumbi wa kanisa la Romani Katoliki, mbele ya wafuasi na wanachama wa vyama hivyo waliokuwa wanasubiri kusikia yaliyofikiwa kwenye kikao hicho.

Wagombea hao walisema wameamua kumaliza tofauti zao baada ya kubaini mgogoro huo utakipa nafasi Chama Chama Mapinduzi kushinda uchaguzi katika jimbo hilo.

Isihaka Mchinjita alisema mgogoro huo ungekinufaisha CCM bila wao kujua kwamba wanakinufaisha chama hicho wakati wanasubiri tamko toka kwa viongozi wa juu wa vyama vyao la kumtangaza kati yao kuwa mgombea.

Alisema kwa kuwa wao ndio waathirika wa mgogoro huo, ndipo wakaamua kutafuta muafaka ambao utasaidia kupambana kwa pamoja kuiondoa CCM katika jimbo hilo, badala ya kuendelea kuhasimiana. 
"Tuliyokubaliana ni mambo mazuri ambayo yamezingatia maslahi ya vyama vyote viwili, tamko rasmi la tuliyokubaliana tutalitoa kwapamoja kwenye mkutano wa hadhara utakaofanyika tarehe 29 mwezi huu," alisema Mchinjita.

Selemani Methew, alisema "ilikulinusuru jimbo lisiangukie mikononi mwa CCM wameamua kufanya jambo ambalo litasababisha lichukuliwa na chama cha upinzani."
Hatuwezi kuendelea kugawanywa wakati lengo letu ni kudiliti CCM(kukifuta Chama Cha Mapinduzi), tulieni wananchi, tuliyokubaliana yanania mzuri mtayafurahia,"alisema Methew.

Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Lindi vijijini, Chikawe Namkaa, alisema wamefikia uamuzi huo ili kurejesha amani katika jimbo hilo kutoka kwenye uhasama uliokuwa na pande tatu. Alisema hali ya usalama katika jimbo hilo imeanza kuwa tete kwa baadhi ya wanachama na wafuasi wa chama chake kuwindwa na kupigwa.
"Mahasimu walikuwa wanatumia mgogoro baina yetu kuwapiga wafuasi wetu nyakati za usiku wakijificha nyuma ya mgogoro huu," alisema Namkaa.

Mwenyekiti huyo alisema watashirikiana na CUF kuweka ulinzi iliwafuasi wapande zote mbili wasidhuriwe na wafuasi wa vyama ambavyo wagombea wake waubunge wanajua hawatashinda na kuamua kukodi wahuni kwenda kuwapiga na kuwatisha wanachama wa chama hicho.
"Tumeondoa tofauti zetu, natutashirikiana katika suala zima la ulinzi, lakini pia makubaliano haya yamefungua mlango wa kutokea ccm kwenye madaraka katika jimbo hili," aliongeza kusema Namkaa.

Mazungumzo ya wagombea hao yaliongozwa na maofisa wa kutoka makao makuu. Ambapo kwa upande wa CUF uliwakilishwa na katibu mkuu wake wa jumuia ya wanawake, Fatma Kalembo, na CHADEMA kiliwakilishwa na Oliver Mwinuka. ambaye ni mratibu wa mikutano na misafara ya mgombea mwenza wa urais kupitia UKAWA, Juma Duni.

About Author

Advertisement

 
Top