Katika hali ya kuhuzunishwa na kile kilichotokea katika Uchaguzi wa kumpata Mgombea ambaye atawakilisha chama cha mapinduzi katika jimbo la Mchinga lililopo Mkoani Lindi, ambalo hata Riziki Lulida alikuwa ni miongoni mwa wagombea.
Lulida aliiambia Lindiyyetu.com wakati wa kupinga matokeo ya Uchaguzi wa Kura za maoni kupitia chama cha mapinduzi Mkoani Lindi katika Hoteli ya Lindi Beach Resort.
Aidha Riziki Lulida anashangaa ni vipi Mgombea ananadiwa na kiongozi wa juu wa chama cha Siasa ambapo ni kinyume na taratibu za chama kama hazikuwa ni Njama zilizopangwa kusababisha wao kushindwa? pia ameweza Kumtaja Mgombea mwingine ambaye yeye ndie alitangazwa kuwa ni Mshindi wa Jimbo hilo kuwa aliweza kuvuruga mkutano wake kwa maandamano makubwa nakusababisha mkutano huo kuvunjika.
Kutokana na kutokea kwa hayoyote na Bado chama cha Mapinduzi hakikuweza kuchukua Hatua stahiki kwa wagombea hao waliovunja taratibu hivyo anashawishika kuwa hakukua na Demokrasia ya kweli na kusema kuwa Uongozi wa chama ulikuwa na wagombea wao waliokuwa wanawataka na sio wao ndio mana chama hakijachukua hatua stahiki.
Amekitaka Chama cha mapinduzi kiweze kusikiliza malalamiko yao ilikukiokoa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu la sivyo yanaweza kujitokeza kama yale yaliojitokeza Uchaguzi mkuu uliopita katika Jimbo la Lindi Mjini ambapo Chama cha Mapinduzi kilipoteza jimbo hilo na kuangukia mikononi mwa Chama cha Wananchi C.U.F
UNAWEZA KUMSIKILIZA HAPA BOFYA PLAY.
RIZIKI LULIDA
Ameweza kueleza jinsi alivyosikitishwa na kauli iliyotolewa na mjumbe mmoja wa kamati ya Siasa ya Mkoa wa Lindi alikwenda katika jukwaa la Siasa na Kumsimamisha Mgombea ambaye alikuwa anamuunga mkono na kutoa kashfa dhidi ya Mgombea yeye Riziki Lulida ambaye ni Mlemavu. Lulida aliiambia Lindiyyetu.com wakati wa kupinga matokeo ya Uchaguzi wa Kura za maoni kupitia chama cha mapinduzi Mkoani Lindi katika Hoteli ya Lindi Beach Resort.