Unknown Unknown Author
Title: MWANAMITINDO MAARUFU, NAOMI CAMPBELL AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIEZI SITA JELA!!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Super Model Naomi Campbell (45) amepatikana na hatia katika kesi iliyokuwa ikimkabili ya kumshambulia mpiga picha. Naomi na aliyekuwa bo...
Super Model Naomi Campbell (45) amepatikana na hatia katika kesi iliyokuwa ikimkabili ya kumshambulia mpiga picha.
Naomi Campbell
Naomi na aliyekuwa boyfriend wake wa wakati huo

Campbell alimpiga Gaetano Di Giovanni jichoni na mkoba wake baada ya mpiga picha huyo kuwapiga picha Campbell na aliyekuwa boyfriend wake wakati huo August, 2009.

Campbell amehukumiwa na Sicilian court kifungo cha miezi sita jela Ijumaa ya July 31, lakini kifungo chake kinafahamika kama "suspended prison term" ambacho hataingia nyuma ya nondo kwa sasa.

"Suspended prison term" ni kifungo ambacho mshtakiwa haendi jela moja kwa moja baada ya hukumu kutolewa, lakini akivunja sheria katika kipindi hicho (miezi sita) ataenda moja kwa moja jela, na akimaliza muda huo bila kufanya kosa wala kuvunja sheria basi anafutiwa mashitaka.

About Author

Advertisement

 
Top