Unknown Unknown Author
Title: MH. BERNARD MEMBE ATEMBELEA BANDA LA BENKI YA NMB KATIKA VIWANJA VYA NANE NANE MKOANI LINDI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
MH. BERNARD MEMBE AKIINGIA KATIKA BANDA LA BENKI YA NMB LILILOPO KATIKA VIWANJA VYA NGONGO KATIKA MAONYESHO YA KILIMO NANE NANE AKIWA AM...
NMB Nane Nane Lindi
MH. BERNARD MEMBE AKIINGIA KATIKA BANDA LA BENKI YA NMB LILILOPO KATIKA VIWANJA VYA NGONGO KATIKA MAONYESHO YA KILIMO NANE NANE AKIWA AMEFUATANA NA OSCA RWECHUNGULA (WAKULIA) PAMOJA NA KAROLI CHANGARO, LEO TAREHE 6.8.2015
NMB Nane Nane Lindi
MH. BERNARD MEMBE AKIPOKEA MAELEKEZO YA BIDHAA ZILIZOZALISHWA NA KIKUNDI CHA MNACHO AMCOS AMBACHO KIMEWEZESHWA NA BENKI YA NMB, MEMBE AKIWA AMEFUATANA NA MKUU WA WILAYA YA RUANGWA Bi. MARIAM MTIMA. LEO TAREHE 6.8.2015
NMB Nane Nane Lindi
MEMBE AKIWA ANAPATA HUDUMA YA KUTOA PESA KATIKA MOJA YA ATM ILIYOPO KATIKA VIWANJA HIVI VYA MAONYESHO YA KILIMO NANE NANE NGONGO MKOANI LINDI MARA ALIPOTEMBELEA BANDA LA BENKI YA NMB LEO TAREHE 6.8.2015


Na. Mwandishi Wetu, Lindi
NMB inashiriki maonyesho ya wakulima ya nane nane katika mikoa saba huku huduma zote za kibenki zikiwa zinafanya kazi katika mabanda yake kama kuweka na kutoa fedha, kupata taarifa za mikopo hasa ya kilimo.

NMB inashiriki maonyesho ya nane nane katika mikoa ifuatayo; Lindi ambako yanafanyika kitaifa, Morogoro, Dodoma, Tabora, Mbeya,Arusha na Kagera.

Wakulima pia wanaotembelea mabanda ya NMB kote nchini watapata fulsa ya kukutana na wataalam wa kilimo na pembejeo, vyama vya ushirika na hivyo kuwa na fulsa nzuri za wao kupata taarifa sahihi na ushauri wa jinsi ya kutumia benki kunufaisha shughuli zao za kilimo.

Kwa kuwa moja ya malengo ya NMB ni kuhakikisha inasaidia ukuaji wa kilimo na kukifanya kuwa cha kibiashara, yenye malengo la kumkwamua mkulima. Hii ni fursa nzuri kwa wakulima, wafanyakazi wa serikali na wajasiriamali kuweza kufika kwenye mabanda ya NMB ili kujionea huduma ambazo benki inatoa.

Kilimo ni uti wa mgongo kutokana na ukweli kwamba karibia 80% ya watanzania wanajishughulisha na kilimo.Kwa kutambua hilo, NMB ipo karibu yao zaidi katika kipindi hiki cha Nane Nane kwa kuleta huduma za kuwanufaisha.
Kauli mbiu ya ‘Kilimo na Mifungo ni biashara’ kwa mwaka huuimeifanya NMB kushirikiana na serikali katika kufanikisha maonyesho ya nane nane katika mikoa yote saba.

Benki ya NMB inatoa huduma mbali mbali za kilimo ikiwa ni pamoja na akaunti maalumu ya Kilimo yaani ‘Kilimo Account’ ambayo inamruhusu mkulima kuweza kujipatia mikopo mbali mbali ili kuweza kuinua uchumi wa Nchi.

NMB Nane Nane Lindi
MH. MEMBE AKIWA NA MKUU WA WILAYA" BERNARD MEMBE AKIPOKEA MAELEKEZO YA HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA BENKI YA NMB KUTOKA KWA OSCA RWECHUNGULA KATIKA BANDA LAO LILILOPO KATIKA SHEREHE ZA MAONYESHO YA KILIMO NANE NANE MKOANI LINDI, MWINGINE NI MKUU WA WILAYA YA RUANGWA Bi. MARIAM MTIMA.
NMB Nane Nane Lindi
MUONEKANO WA BANDA

About Author

Advertisement

 
Top