Unknown Unknown Author
Title: CHELSEA YASHINDWA KUTAMBA MBELE YA PSG, YASHINDA KWA MIKWAJU YA PENALTI 6-5
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya Chelsea imeshindwa kutamba mbele ya PSG ilipokubali kulazimishwa kutoka sare ya Goli 1-1, Hivyo kupelekea Mchezo huo kuamuliwa kwa ...
Timu ya Chelsea imeshindwa kutamba mbele ya PSG ilipokubali kulazimishwa kutoka sare ya Goli 1-1, Hivyo kupelekea Mchezo huo kuamuliwa kwa mikwaju ya Penalti huku kipa wa Chelsea Thibaut Courtois kuibuka shujaa wa mchezo huo mara Baada ya Kuokoa mikwaju miwili ya Penalti.
Chelsea Vs PSG
Zlatan Ibrahimovic ndiye alikuwa wakwanza kuifungia timu yake ya PSG Goli la kwanza katika mchezo huo mnamo dakika ya 24 ya Mchezo huo mara baada ya kufanyika kwa makosa ya mabeki wa Timu ya Chelsea.

Kipindi cha Pili Timu zote zilifanya Mabadiliko na katika Upande wa Chelsea waliweza kuwatoa Begovic, Mikel and Cahill na waliochukua nafasi zao walikuwa  Courtois, Zouma and Ramires. Na upande wa PSG waliotoka walikuwa Luiz, Verratti and Stambouli ambapo nafasi zao zilichukuliwa na Marquinhos, Motta and Rabiot.
Chelsea Vs PSG
Mnamo dakika ya 64 ya kipindi cha pili ni Victor Mosses aliefunga goli la kusawazisha baada ya kupokea pasi maridhawa kutoka kwa Cesc Fabregas Hadi dakika tisini zinakamilika matokeo yalibaki kuwa 1-1 na kuamuliwa kupigwa mikwaju ya Penalti ambapo Chelsea ilishinda kwa mikwaju 6-5.

Katika mchezo wa Awali Timu ya Chelsea walifungwa Goli 4-2 na Timu ya New York RedBulls. PSG wao waliweza ishinda Fiorentina kwa jumla ya Goli 4-2. Katika mshindano hayo ya International Champions Cup

About Author

Advertisement

 
Top