YANGA SC YASAJILI KIFAA KINGINE CHA KIMATAIFA, DIDA AKIONGEZA MKATABA WAKE KWA MIAKA 2

Mshambuliaji wa kimataifa Donald Ngoma "Dombo" anatarajiwa kutua muda wowote katika klabu ya Yanga kuanza kuitumikia klabu hiyo mara baada ya michuano ya COSAFA kumalizika, mshambuliaji huyo tegemeo la Zimbabwe na klabu ya FC Platnum amemalizana na Yanga kila kitu huku atasaini mkataba wa miaka 2.
Mwinyi Hadji Mngwali na Donald Ngoma
Mhezaji huyo mwenye nguvu, chenga, mbio, mashuti na uwezo mkubwa wa ku control mpira atatua kuja kuunda safu kali ya ushambuliaji sambamba na mrundi Amiss Tambwe.

Wakati huo huo beki wa Taifa stars Mwinyi Hadji Mngwali ambaye huchezea klabu ya KMKM amesajiliwa kuichezea Yanga huku tukio hilo likiambatana na Deo Dida kusaini mkataba wa miaka 2 baada ya ule wa awali kumalizika!
Previous Post Next Post