SHILOLE BADO HALI TETE NA TUKIO LA UBELGIJI, SERIKALI YAPANIA KUMCHUKULIA HATUA

Serikali imeahidi kumchukulia hatua Shilole kufuatia kusambaa kwa picha zake chafu zilizopigwa wakati akitumbuiza nchini Ubelgiji.
Shilole
Akizungumza bungeni Dodoma leo, Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Juma Mkamia, wakati akijibu hoja za wabunge baada ya kusoma makadirio na matumizi wa wizara hiyo, alisema tayari serikali imeliagiza baraza la sanaa taifa BASATA kufanya naye mahojiano.

 Juma MkamiaNaibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Juma Mkamia

“Tumemtaka ajieleze kupitia BASATA, akishajieleza serikali itachukua hatua na niombe mheshimiwa spika kupitia bunge lako tufuku, kuliomba radhi kwa upande wa serikali kwa kitendo kilichofanywa na mwanamuziki yule. Sio maadili yetu na nimesema akishajieleza serikali itachukua hatua yake,” alisema Juma Mkamia.
Previous Post Next Post