Bosi wa Manchester United Louis van Gaal amesema Klabu yao inajua nani wanaweza kumbadili Kipa wao David De Gea akiamua kuihama Old Trafford.
Akiongea hapo Jana, Van Gaal amesema hajui kama Kipa huyo mwenye Miaka 24 atabaki au la lakini wao wana mipango ikiwa ataondoka.
Van Gaal amesema: "Tunayo Listi ya Makipa wanaoweza kumbadili kwa sababu lazima tuwe tayari Siku zote!"
Huku kukiwa na habari zilizozagaa kuwa Kipa huyo anarudi kwao Spain kujiunga na Real Madrid, Man United ilitoa Ofa ya Mkataba mnono kwa Kipa huyo na mazungumzo yamekuwa yakiendelea.
Van Gaal ameeleza: "Tunataka abaki na tunategemea atasaini."
Hata hivyo, Van Gaal amesema Mtu pekee atakaeamua hatima yake ni De Gea pekee na si yeye wala Klabu.
Tayari kwa ajili ya Msimu ujao, Man United imeshamsaini Fowadi wa Holland, Memphis Depay, kutoka PSV Eindhoven na Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Ed Woodward, ameahidi Wachezaji wengine wapya wapo njiani kununuliwa.
Pia Van Gaal alihojiwa kuhusu Straika wa Tottenham Harry Kane na Winga wa Wales anaechezea Real Madrid Gareth Bale, na kujibu: "Naona nahusishwa na kununua kila Mtu Duniani lakini sivyo hivyo!"
MSIMAMO-TIMU ZA JUU: LIGI KUU ENGLAND
**Mechi zilizochezwa/Tofauti ya Magoli/Pointi
Mkataba wa De Gea na Man United unamalizika mwishoni mwa Msimu ujao, ule wa 2015/16, na Kipa huyo bado hajaamua kusaini Mkataba mpya ambao ameshapewa Ofa yake.
Akiongea hapo Jana, Van Gaal amesema hajui kama Kipa huyo mwenye Miaka 24 atabaki au la lakini wao wana mipango ikiwa ataondoka.
Van Gaal amesema: "Tunayo Listi ya Makipa wanaoweza kumbadili kwa sababu lazima tuwe tayari Siku zote!"
Huku kukiwa na habari zilizozagaa kuwa Kipa huyo anarudi kwao Spain kujiunga na Real Madrid, Man United ilitoa Ofa ya Mkataba mnono kwa Kipa huyo na mazungumzo yamekuwa yakiendelea.
Van Gaal ameeleza: "Tunataka abaki na tunategemea atasaini."
Hata hivyo, Van Gaal amesema Mtu pekee atakaeamua hatima yake ni De Gea pekee na si yeye wala Klabu.
Tayari kwa ajili ya Msimu ujao, Man United imeshamsaini Fowadi wa Holland, Memphis Depay, kutoka PSV Eindhoven na Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Ed Woodward, ameahidi Wachezaji wengine wapya wapo njiani kununuliwa.
Pia Van Gaal alihojiwa kuhusu Straika wa Tottenham Harry Kane na Winga wa Wales anaechezea Real Madrid Gareth Bale, na kujibu: "Naona nahusishwa na kununua kila Mtu Duniani lakini sivyo hivyo!"
MSIMAMO-TIMU ZA JUU: LIGI KUU ENGLAND
**Mechi zilizochezwa/Tofauti ya Magoli/Pointi
- Chelsea 36/42/84
- Man City 36/41/73
- Arsenal 35/32/70
- Man United 36/25/68
- Liverpool 36/11/62
- Tottenham 36/2/58
- Southampton 36/18/57