Sweetbert Lukonge,Dar es Salaam
STRAIKA wa Yanga, Amissi Tambwe aliondoka nchini hivi karibuni kwenda kwao Burundi kwa mapumziko, hali aliyokutana nayo huko si nzuri na imemlazimu kulikimbia Jiji la Bujumbura na kwenda Kijiji cha Makamba jirani na mpaka wa Tanzania kwa usalama zaidi.
Wasiomuunga mkono Rais Pierre Nkurunziza wakiongozwa na Meja Jenerali, Godefroid Bniyombareh, walitangaza kuipindua serikali ya Burundi chini ya Rais Nkurunziza wakipinga mpango wa rais huyo kuwania kwa mara ya tatu urais wa nchi hiyo kinyume na katiba.

Straika wa Yanga, Amissi Tambwe.
Akizungumza na Championi Jumamosi kutoka Makamba, Tambwe alisema sehemu aliyokuwa anaishi jijini Bujumbura imekumbwa na ghasia za mara kwa mara, hivyo familia kuwa hatarini ndipo alipoamua kuhamia Makamba.
“Imebidi niiondoe familia yangu Bujumbura na sasa ipo Makamba mpakani mwa Tanzania na Burundi ambapo ndipo lilipo chimbuko letu kwa ajili ya usalama zaidi kwani hali si nzuri huko tulikotoka.
“Kijijini hapa hali ni shwari hivyo tutarudi Bujumbura pindi mambo yatakapokuwa sawa ili mwanangu, Froly aendelee na masomo. Kama tungebaki Bujumbura lolote lingeweza kutokea kwani watu wanapigana hovyo na majeshi ya serikali yanatuliza maandamano kwa nguvu kubwa,” alisema Tambwe.
Mpaka sasa zaidi ya watu 100,000 wameikimbia Burundi na kuingia Tanzania na Rwanda kuomba hifadhi kwa usalama wao na watu kadhaa wameripotiwa kufa kutokana na maandamano.Maandamano hayo yanapinga kitendo cha Chama cha CNDD- FDD kumtangaza Nkurunziza kuwa mgombea wake wa urais kwa muhula wa tatu.

Tags
SPORTS NEWS