BIFU LA WEMA SEPETU NA AUNT EZEKIEL LAFIKIA PABAYA, WATOLEANA KAULI NZITO...!!!

Hivi karibuni, baada ya kuvunjika kwa urafiki wa ‘kupika na kupakua’ kati ya mashostito wawili walio katika tasnia ya Bongo Movies, Aunt Ezekiel Grayson na Wema Isaac Sepetu wametoa maneno makali ambayo yametumika pasipo sababu.
Aunt Ezikiel na Wema
Juzi, Aunt ameibuka na kutoa kauli kali bila kuuma maneno kwamba, Wema akitangulia kuaga dunia, yeye hatakwenda kumzika kwa maana ya kuuaga mwili wake sanjari na kuomboleza.

Kauli hiyo ya Aunt imekuja siku chache baada ya Wema naye kudaiwa kutoa kauli kama hiyo akisema kwamba, kutokana na urafiki wake na Aunt kufa na kuwa maadui, basi hata akifa, Aunt asiende kumzika.
Aunt Ezikiel na Wema

MAHOJIANO:MSIKIE AUNT ‘LAIVU’
Mwandishi: Aunt pole kwa kulea mimba! Nina machache sana. Wema amedaiwa kuanika hatima ya ugomvi wenu kwamba, hali ilipofikia hata akifa wewe usiende kumzika. Wewe unasemaje?
Aunt: Kwanza nashangaa taarifa za kwamba nina ugomvi na Wema maana hata hao ndugu zake nimesikia wanaongea mambo kibao.

“Ila mimi sioni kama kuweka picha ya tangazo la shoo ya Zari (Zarinah Hassan) kwenye peji yangu ya Instagram ni kosa. Kwa hiyo kama yeye hataki kuzikwa na mimi, hata mimi nasema sitamzika Wema.
”Halafu sidhani kama kuna mtu anaweza kunipangia kitu kwenye peji yangu mwenyewe ambayo nina uamuzi wa kufanya chochote ninachojisikia.
“Mimi sidhani kama hapo kuna ugomvi, maana nilichoandika na kuweka siku hiyo ilikuwa ni utani lakini hata kama yeye na ndugu zake walichukulia ‘siriasi’ basi bado walitakiwa kutambua kuwa, mchumba wangu Iyobo (Moses) ni mfanyakazi halali wa kundi la muziki la Diamond (Nasibu Abdul), hivyo nilikuwa na haki ya kumsapoti kwa asilimia zote maana fedha anazopata kupitia huko ndizo zinazonifanya mimi na familia yangu niishi,”
alisema Aunt.
Aunt Ezikiel na Wema
Aunt alizidi kufunguka baada ya kuambiwa kuhusu maazimio ya kikao cha familia ya Wema ambacho kilimtaka wema asiwekaribu tena na Staa huyo alisema:
“Kama familia yake wamefikia hatua ya kuingilia hili, mimi nafikiri sina tatizo maana nina maisha yangu na yeye (Wema) ana maisha yake. Ila tu kama ni ishu ya wazazi, naomba wajue pia mimi sijajizaa wala sijazaliwa na miti, nina ndugu tena wanajitambua kwa kila hali.
“Nikiangalia sababu za ugomvi ni za kibinafsi sana hata hazifai kuingiliwa na mtu, maana haiwezekani kwenye maisha haya eti Wema akinuniana na mtu basi na mimi nimnunie, sijaumbwa hivyo wala sina unafiki huo.
“Kama staili ya maisha ikiwa kila atakayekwazana naye na mimi nimchukie siku wanapoelewana mimi si nitaonekana sifai kote? Wao wafahamu kuwa mimi najitambua wala si wa kuburuzwa hivyo.
“Kama wanasema hawawezi kushiriki lolote kwangu hata mimi sina sababu ya kujipendekeza kwao.
“Hakuna kitu kibaya katika maisha kama kuwa na rafiki ambaye siku zote yeye akikosana na mtu basi na wewe ukosane naye. Mbona mimi maadui zangu yeye ni marafiki zake na wala sijawahi kununa. Iweje sisi tukorofishane na watu yeye aongee nao ila yeye akikorofishana na watu basi hataki kabisa hata kutuona nao?”
Aunt Ezikiel na Wema
WEMA NAYE ATEMA NENO
Baada ya MWANDISHI kupata fukunyuku hizo alimsaka Wema kwa maana ya kujiridhisha na kinachodaiwa kusemwa na yeye na familia yake, mambo yalikuwa hivi:
“Yaani hata sitamani kusikia jina la Aunt maana alichokifanya ni bora hata ya Kajala ambaye ishu yake ni ya moja kwa moja. Nashindwa kuliweka wazi sana lakini familia yangu haitaki hata kumsikia kwa jinsi ilivyochukizwa naye.
“Sifikirii kama kuna siku nitakuja kukaa naye tena au kuongea chochote mbele yake maana alichokifanya si cha kunifanyia mimi tuliyeshibana kama mapacha.”


Aunt ‘mama kijacho’ na Wema walikuwa marafiki walioshibana kabla ya kutofautiana baada ya Aunt kutoa sapoti kwa mpenzi wa Diamond, Zari kwenye shoo yake ya Zari All White Party kwa kuposti picha kwenye mtandao iliyoonesha kupigia debe shughuli hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Mlimani City hivi karibuni jambo lililomkera Wema akiamini Aunt ni mnafiki, yuko kwake na kwa mahasimu wake hao.
>>GPL
Previous Post Next Post