Unknown Unknown Author
Title: WAETHIOPIA HARAMU WALIOKAMATWA APRIL 14 MITWERO-LINDI, WATUPWA JELA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
WATUHUMIWA WAKISHUKA KWENYE GARI KITUO CHA POLISI LINDI MARA BAADA YA KUKAMATWA TAREHE 14/04/2015, MITWERO -  LINDI Na Abdulaziz Lind...
Kituo cha Polisi - Lindi
WATUHUMIWA WAKISHUKA KWENYE GARI KITUO CHA POLISI LINDI MARA BAADA YA KUKAMATWA TAREHE 14/04/2015, MITWERO -  LINDI

Na Abdulaziz Lindi
MAHAKAMA ya wilaya ya Lindi,imewahukumu watu (34) raia wa Ethiopia kifungo cha miezi sita Jela kila mmoja, baada ya kupatikana na hatia ya kuingia na kuishi nchini kinyume cha Sheria.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, Aluu Nzowa, kufuatia washitakiwa hao waliokuwa wakiongozwa na mkalimani, Mulgheta Shirmai, kukiri makosa yaliyokuwa yanawakabiri.

Waliohukumiwa ni,Yissak Bonge Mulgeta (22), Faranji Lewaro (22), Mulgeta Dabala (23), Mogos Ayale (20), Paulos Desta (19), Aniso Adise (21), Malese Adir (19), Jashale Handebo (17), Ision Zaleke (18), Habtamo Wolde (20), Damake Mulata (20), Misgana Alam (19) na Elias Desta (20).

Wengine ni, Mulatu Kabada (18), Jasphaya Erago (18),I syas Emmanuel (25), Ergudo Abbo (18), Alamayo Dagalo (18), Malasa Diga (20), Erimako Marcos (18), Tadela Eriso (20), Ana Mugole (19), Tarakin Mathias (18), Sinot Masala (20), Matiwo Tadiso (23), Takatali Lolamo (20) na Adise Anito (16).

Aidha,wengine ni, Muses Awolo (17), Endala Ebara (20), Maluku Tamiratu (20), Nuguse Horamo (15), Michael Elifene (20), Dilamo Afiricho (16) na Habtamu Matwos (17) wote ni raia wa Ethiopita.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo,washitakiwa hao kupitia mkali mani wao huyo, walipewa nafasi ya kujitetea ambapo kila mmoja aliiomba mahakama hiyo, iwaonee huruma kwani ni wakosaji wa mara ya kwanza, pia wao sio lengo lao kuishi Tanzania bali walikuwa wanapita njia kuelekea nchi jirani ya Msumbiji.

Baada ya kusikiliza utetezi huo, Hakimu Nzowa alimuuliza mwanasheria wa Serikali Juma Maige, kama anakumbukumbu ya makosa ya zamani kwa washitakiwa hao, ambapo alijibu hana, kisha kuiomba mahakama kuangalia hukumu itakayowafaa.

Hakimu Nzowa akitoa hukumu katika kesi hiyo namba 43/2015, aliwahukumu kila mmoja kulipa faini ya Sh, 50,000/- na watakapo shindwa watalazimika kutumikia kifungo cha miezi sita Jela, kila mmoja, na pale watakapomaliza adhabu warudishwe nchini kwao Ethiopia.

Washitakiwa hadi waandishi wanaondoka kwenye viwanja hivyo vya mahakama,walikuwa bado hata mmoja aliyejitokeza kulipa faini walizohukumiwa.

Awali ilidaiwa mahakamani hapo na mwanasheria wa Serikali Juma Maige, kuwa washitakiwa wote kwa pamoja walikamatwa April 14 mwaka huu, mtaa wa mitwero, wakiwa wamehifadhiwa na baadhi ya wenyeji, kwenye korongo la mlima mmongo ndani ya Manispaa ya Lindi, wakisubiri taratibu zingine za kuendelea na safari yao kuelekea nchini Msumbiji.

About Author

Advertisement

 
Top