CRISTIANO RONALDO AONDOLEWA ADHABU, SASA KUCHEZA KESHO DHIDI YA EIBAR

Mshambuliaji Cristiano Ronaldo ameondolewa adhabu ya kutocheza mchezo wa mwishoni mwa juma hili baada ya rufaa ya uongozi wa Real Madrid kufanikiwa.
Cristiano Ronaldo
Kanuni za ligi ya nchini Hispania zilikua zinambana Ronaldo kucheza katika mchezo wa kesho dhidi ya Eibar, kutokana na kufikisha idadi ya kadi tano za njano, mara baada ya mchezo wa siku mbili zilizopita ambapo Real Madrid walichomoza na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri dhidi ya Rayo Vallecano.

Uongozi wa Real Madrid uliwasilisha rufaa ya kupinga maamuzi yaliyochukuliwa na muamuzi aliyechezesha mchezo dhidi ya Rayo Vallecano, sambamba na ushahidi wa tukio la kuanguka katika eneo la kisanduku cha penati ambapo alidhaniwa alifanya makusudi.

Kamati ya mashindano iliyo chini ya shirikisho la soka nchini Hispania imejiridhisha kutokana na ushahidi, na imebainika Ronaldo hakujiangusha kwa makusudi bali alichezewa ndivyo sivyo na beki wa Rayo Vallecano, Antonio Amaya katika dakika ya 51.

Kwa mantiki hiyo sasa Ronaldo atakuwa sehemu ya kikosi cha Real Madrid kitakachoshuka kwenye uwanja wa nyumbani hiyo kesho kupambana dhidi ya Eibar.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post