Unknown Unknown Author
Title: CHADEMA YAITAKA NEC KUTANGAZA TAREHE RASMI YA ZOEZI LA KURA YA MAONI YA KATIBA PENDEKEZWA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Chama cha Demokrasia na maendeleo ( CHADEMA ) kimemtaka mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi ( NEC ),jaji mstaafu Damian Lubuva kutang...
Damian Lubuva
Chama cha Demokrasia na maendeleo ( CHADEMA ) kimemtaka mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi ( NEC ),jaji mstaafu Damian Lubuva kutangaza tarehe rasmi ya zoezi la kupiga kura ya maoni kwa katiba inayopendekezwa ili kuwaondoa wananchi katika hali ya sintofahamu, baada ya zoezi hilo kuahairishwa kwa muda usiojulikana kutokana na kutokamilika kwa uandikishaji upya wa daftari la kudumu la wapiga kura.

Aprili 2 mwaka huu tume ya taifa ya uchaguzi ilitangaza kuahairisha tarehe ya kupigia kura ya maoni katiba inayopendekezwa iliyopangwa kufanyika aprili 30, licha ya tume hiyo kuelezwa tangu awali na wadau kuwa haitawezekana kura ya maoni kufanyika tarehe hiyo kama ilivyokuwa imetangazwa awali na Rais Jakaya Kikwete.

Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza la wazee wa chadema wilaya ya ilemela mhandisi Vedasto Patrick amevitaka vyama vya siasa nchini kusimamia amani na utulivu uliopo nchini, kwani amani ni zaidi ya jambo lolote na inahitaji kulindwa na kila mtanzania ili kulinusuru taifa kuingia katika machafuko yanayotokea hivi sasa katika mataifa mengine.

Kuhusu mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi – ALBINO yaliyopoteza maisha ya watu 76 nchini, wakiwemo watu 15 wa mkoa wa Mwanza huku wengine 50 wakiwa wamepoteza viungo mbalimbali vya miili yao, mweka hazina wa chadema wilaya ya ilemela Edwin Sarungi amesema kuamini kuwa viungo vya Albino vinasaidia kupata madini, madaraka ya kisiasa pamoja na kuleta utajiri, ni imani potofu, za kishetani, kifedhuli, kijinga na za kipuuzi huku mwenyekiti wa Bavicha wilayani humo John Memba akiwahimiza wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura muda utakapowadia.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top