Unknown Unknown Author
Title: ALLY CHOCKY NA SUPER NYAMWELA WAREJEA NYUMBANI TWANGA PEPETA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kiongozi wa Twanga Pepeta, luixa Mbutu akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo. Kulia ni Choki na (kushoto), ni Super Nyam...
Twanga Pepeta
Kiongozi wa Twanga Pepeta, luixa Mbutu akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo. Kulia ni Choki na (kushoto), ni Super Nyamwela. PICHA/HISANI YA SALUTI5

Na. Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Mwanamuziki wa dansi mkongwe nchini, Ally Chocky amejiunga rasmi na African Stars wana Twanga Pepeta.

Chocky alitangazwa leo na uongozi wa Twanga Pepeta katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hoteli ya Nemax iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Aidha Chocky amejiunga pamoja na mcheza shoo mkongwe Super Nyamwela.

Onyesho la kwanza la Chocky katika bendi hiyo litakuwa tarehe 18 mwezi huu, katika ukumbi ambao utatangazwa baadae.

“Tayari nna tungo tatu nitakazoanza nazo ambazo ni ‘Usiyaogope maisha’, ‘Kichwa chini’ na ‘No discussion’," alibainisha Chocky katika mkutano huo.

Mkutano huo pia ulihudhuliwa na Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka na Kiongozi wa bendi hiyo, Luiza Mbutu.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top