MWILI WA MAREHEMU ABDUL BONGE WAHAMISHIWA HOSPITALI YA MUHIMBILI KWA UCHUNGUZI ZAIDI

Marehemu Abdul BongeMwili wa Abdu Bonge ukitolewa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mwanyamala jijini Dar ili kuhamishiwa Muhimbili.
Marehemu Abdul Bonge…Ukiwa ndani ya gari kwa ajili ya kupelekwa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.
Marehemu Abdul Bonge
Safari ilivyoanza kuelekea Muhimbili.

MWILI wa aliyekuwa mwanzilishi wa Kundi la Tip Top Connection, Abdu Bonge, mapema leo asubuhi ulihamishwa kutoka katika Hospitali ya Mwananyamala na kupelekwa Muhimbili kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi.

Mtandao huu ulishuhudia jamaa wa marehemu huyo wakiuhamisha mwili huo wakisema ni lazima mwili huo ukafanyiwe uchunguzi wa kina kutokana na utata wa kifo chake.

Mdogo wa marehemu aitwae Idd Taletale alisema endapo uchunguzi huo utamalizika leo utasafirishwa leo kuelekea Kijiji cha Mkuyuni kilichopo Matombo mkoani Morogoro kwa ajili ya mazishi.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post