Unknown Unknown Author
Title: MAJAMBAZI WANNE (4) MBARONI KWA MAUAJI MKOANI DODOMA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SA...
Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limewakamata majambazi wanne (4) waliomuua ASHELI S/O MAGINA mwenye miaka 40, Msukuma, Mfanyabiashara/Mkulima wa Kijiji cha Bubutole kwa kumkata na mapanga kichwani na mikononi na kufariki papo hapo tukio lililotokea tarehe 11/02/2015 majira ya saa 02:00hrs usiku katika Kijiji cha Bubutole Kata ya Farkwa, Tarafa ya Farkwa Wilaya ya Chemba Mkoani humo.

Amewataja majambazi hao waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo kuwa ni:

1. HASSAN S/O MAULIDI @ SALAMA, mwenye miaka 32, kabila Msandawe, Mkulima.
2. HAMADI S/O HUSSEIN mwenye miaka 25, kabila Msandawe, Mkulima.
3. RASHID S/O YUSUPH, mwenye miaka 21, kabila Msandewe, Mkulima.
4. ABDALAH S/O SWALEHE @MUNA, mwenye miaka 25, kabila Msandawe, Mkulima, wote wakazi wa Kijiji cha Porobanguma Wilayani Chemba Dodoma.

Kamanda MISIME amefafanu kuwa majambazi hao walimvamia ASHELI s/o MAGINA nyumbani kwake akiwa amelala dukani na kumshambulia kwa mapanga na kufariki dunia kisha kupora mali mbalimbali ikiwemo pikipiki, mifuko miwili ya sukari ya kilo 25, mifuko miwili ya unga wa ngano ya kilo 25 na soda kreti tatu(3) mali ambayo thamani yake haijafahamika.

Ameendelea kusema kwamba majambazi hao walikamatwa wakiwa na pikipiki yenye namba T. 449 CQP aina ya SUNLG mali ya marehemu waliyopora eneo la tukio na baadhi ya mali walizopora kama sukari na maharage. Pia waliweza kuonyesha mapanga waliyotumia kumkatakata nayo ASHELI s/o MAGINA.

Aidha Kamanda MISIME amesema mtuhumiwa HASSAN s/o MAULIDI @ SALAMA alikuwa anatafutwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la mauaji ya IJUMAA S/O SAID mwenye miaka 30, Msandawe Mkulima na Mkazi wa Kijiji cha Monjore Banguma kwa kumchoma na kisu tukio lililotokea tarehe 19/01/2015 majira ya saa 18:30hrs katika kijiji cha Porobanguma kwa kile kilichodaiwa kua ni ugomvi uliyotokea baina yao. Uchunguzi zaidi unaendelea na ukikamilika watafikishwa mahakamani.

Kamanda MISIME ametoa wito kwa Wananchi waendelee kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu, kwani wahalifu wanaishi katika jamii na kufanya uhalifu ndani ya jamii. Wahalifu wasifumbiwe macho.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top