Unknown Unknown Author
Title: BAJETI YA WILAYA YA KILWA NI BILIONI 27.4 KWA MWAKA 2015/2016
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wajumbe wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya Kilwa Mkoani Lindi wakiwa kikaoni cha Bajeti Diwani wa Lihimalyao Mahadhi Nango...

BARAZA LA MADIWANI KILWA
Wajumbe wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya Kilwa Mkoani Lindi wakiwa kikaoni cha Bajeti
BARAZA LA MADIWANI KILWA
Diwani wa Lihimalyao Mahadhi Nangoma akichangia suala la makusanyo wa fedha za bima ya afya CHF katika wilaya hiyo
BARAZA LA MADIWANI KILWA
Mwanasheria wa Halmshauri ya Wilaya Kilwa na Afisa Utumishi wakiwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wakifuatilia kikao hicho kwa umakini


Mwandishi wetu Kilwa
Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mkoa wa Lindi, lilipitisha mpango wa makisio ya bajeti mwenye jumla ya Shilingi Bilioni 27.4 kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016.

Akisoma bajeti hiyo Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo, Maimuna Mtanda alisema katika kipindi hicho Halmashauri hiyo itahitaji kuwa na jumla ya shilingi 27,419,533,212.00 ambazo zitatumika katika kutekeleza miradi ya maendeleo na matumizi ya kawaida (mengineyo) na mishahara ya watumishi.


Mtanda alisema bajeti hiyo ina ongezeko la shilingi 6,420,907,082.00 sawa na asilimia 30.6 ya bajeti ya mwaka 2014/2015 kutokana na ongezeko la mishahara yenye jumla ya shilingi 6,403,484,812.00,sawa na asilimia 58.8 ya mishahara ya bajeti iliyopita, na ongezeko la mapato ya ndani lenye jumla ya shilingi 17,422,270.00.

Alisema kuwa fedha hizo zitatokana na makusanyo kwenye vyanzo mbalimba ikiwa ni pamoja na ruzuku ya mishahara shilingi 18,300,146,812.00, ruzuku ya matumizi mengineyo shilingi 1,617,843,000.00, ruzuku ya miradi ya maendeleo shilingi 3,161,080,000.00, mapato ya ndani shilingi 2,823,047,400.00 na misaada kutoka kwa wahisani na marafiki wa maendeleo shilingi 1,472,416,000.00.

Mtanda alisema ili kuongeza kiwango cha mapato ya ndani Halmashauri hiyo imeandaa mikakati ya ukusanyaji mapato, ikiwamo kuanzisha kikosi kazi cha ukusanyaji mapato, kuongeza wigo wa kubuni vyanzo vipya vya mapato, kuongeza viwango vya kodi katika baadhi ya vyanzo vya mapato na kuimarisha rejesta za vyanzo mbalimbali vya mapato.

Mkurugenzi huyo alisema katika matumizi ya shughuli za maendeleo kipaumbele kitakuwa kutekeleza miradi ya maji, kwani katika wilaya ya hiyo ni asilimia 47 ya wananchi wanaopata na kutumia maji safi na salama.

Kwa upande wake katibu tawala msaidizi wa mkoa Lindi, Abdallah Dachi aliitaka Halmashauri hiyo kuwa na udhibiti na ukusanyaji wa mapato, ambapo pia aliitaka kuipa vipaumbele miradi ambayo haijakamilika (viporo).

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top