Unknown Unknown Author
Title: AFISA MTENDAJI MKUU WA TTCL, AFANYA ZIARA YA MIKOA YA KUSINI NA NYANDA ZA JUU KUSINI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura akikagua mitambo ya TTCL mkoani Lindi. Afisa Mtendaji Mkuu Dr Kamugisha Kazaura atembelea mik...
TTCL mkoa wa Lindi
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura akikagua mitambo ya TTCL mkoani Lindi.

Afisa Mtendaji Mkuu Dr Kamugisha Kazaura atembelea mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Mbeya ikiwa na lengo la kukagua miundombinu ya TTCL na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano pamoja na kuzungumza na wafanyakazi wa TTCL wa mikoa hiyo.

Dr Kazaura ailijionea juhudi mbalimbali zinazofanywa na wafanyakazi wa TTCL katika kuhakikisha miundombinu ya TTCL na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano inakuwa salama muda.

Hivi sasa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) imekuwa kampuni pekee ya mawasiliano ambayo imefanikiwa kuunganisha wateja mbalimbali kupitia mtandao wake.

Wateja hao ni pamoja na TAMISEMI, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA), Mabenki, Wizara ya Afya, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabau za Serikali (CAG),Wizara ya Fedha, watoa huduma za mtandao/intaneti (ISPs) pamoja Makampuni ya Simu

Pia TTCL imefanikiwa kuunganisha nchi jirani katika ukanda huu wa afrika Mashariki (Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda) pamoja na nchi za kusini wa Jangwa la Sahara (SADC) ambazo ni Malawi na Zambia.

TTCL mkoa wa Lindi
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura akipokea maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa TTCL Mtwara kuhusu juhudi zinazofanyika kulinda na kusimamia mitambo yake.
TTCL mkoa wa Lindi
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura akikagua Mtambo wa Mkongo wa Taifa, pembeni yake ni Mkuu wa Idara ya Ufundi wa TTCL,Senzige Kisenge.
TTCL mkoa wa Lindi
Meneja wa TTCL mkoa wa Lindi- John Nindwa akimuonesha Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura eneo ambalo Mkongo wa Taifa ulikatwa na wezi katika hifadhi za Taifa ya Selous na juhudi zilizofanyika katika kurejesha mawasiliano Ruvuma.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top