KINANA AWATAKA VIONGOZI WA DINI KUIKEMEA CUF KUWAITA MAKAFIRI WANAOHAMIA CCM

Kinana - Chake Chake Pemba
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman, akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Pujini wilayani Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Katika mkutano huo, Kinana alitumia staili yake ya kuwakataza wananchi kumshangilia akiwataka wamsikilize vizuri maneno aliyokuwa akizungumza kuhusu utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ambapo alimsifia Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein kwa uchapakazi wake kwa kuwaletea maendeleo wananchi katika visiwa vya Pemba na Unguja.

Alisema wakati wa uongozi wake amejenga barabara nyingi za lami, miradi ya maji, Afya na elimu karibu kila kona ya visiwa vya Pemba na Unguja, lakini wakati anafanya mambo yote hayo wapinzani wakiwemo viongozi wa CUF na wafuasi wao wanajifanya hawayaoni maendeleo hayo.

Alisema Serikali YA ccm iliyo chini ya Rais Dk. Shein imepeleka umeme, miradi ya maji na barabara za lami hata katika Jimbo la Mtambwe alikozaliwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad.

Kinana amelaani kitendo cha CUF kuwaita makafiri watu wotinginee wanaokihama hicho kwenda CCM na vyama vingine, ambapo ameomba viongozi wa dini kulikemea jambo hilo, akidai hakuna binadamu mwenye haki ya kumwita mwenzie kafiri isipokuwa Mungu.

Pia alikemea vikali tabia isiyo sahihi iliyozuka ya kuwatenga waliokuwa wana CUF na kuamua kujiunga na CCM na vyama vingine, akidai kila mtu ana haki ya kujiunga na chama chochote akipendacho. 

Kinana - Chake Chake Pemba
Wananchi wakishangilia wakati Kinana akiingia kuhutubia katika mkutano huo.
Kinana - Chake Chake Pemba
Aliyekuwa Mwanachama wa CUF na kuhamia CCM, Gharib Bedui Hamisi akionesha kadi yake kabla ya kumkabidhi Komredi Kinana aliyemkabidhi kadi ya CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Pujini, Chakechake, Pemba. Hamis alielezea katika mkutano huo kuwa baada ya kutangaza kuhamia CCM AMATENGWA NA FAMILIA YAKE PAMOJA NA BAADHI YA MARAFIKI ZAKE.
Kinana - Chake Chake Pemba
Kinana akishiriki ujenzi wa jengo la CCM tawi la Mchangani Jimbo la Wawi.Wilaya ya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba.
Kinana - Chake Chake Pemba
Kinana akishiriki kuotesha miche ya mikarafuu katika shamba la Kikundi cha Hatukosani Jimbo la Chakechake
Kinana - Chake Chake Pemba
Kinana akipanda mti  akatika shamba la miti la Ushirika wa Hatugombani, Shaia ya Kilindi, Chakechake, Pemba

1 Comments

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

  1. kinana naona wewe ndio kiongozi bora ya ccm, kwa hiyo endelea kuimarisha chama tawala.

    ReplyDelete
Previous Post Next Post