Unknown Unknown Author
Title: CHANZO CHA KIWANGO CHA MCHEZAJI WA YANGA "MRISHO NGASA" KUSHUKA CHAWEKWA HADHARANI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mrisho Ngassa Kuendelea kukatwa makato makubwa imeelezwa ndiyo chanzo cha kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa , kudorora uwanj...
Mrisho Ngassa
Mrisho Ngassa
Kuendelea kukatwa makato makubwa imeelezwa ndiyo chanzo cha kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa, kudorora uwanjani.

Ngassa amekuwa kwenye kiwango cha chini msimu huu ikiwa ni tofauti na misimu mingine yote iliyotangulia. 

Kiungo huyo, alitua kuichezea timu hiyo kwenye msimu wa 2013/2014, kwa makubaliano ya kulipa fedha shilingi milioni 45, ikiwa ni deni la shilingi milioni 30 pamoja na faini ya milioni 15 za Simba ili aweze kuitumikia timu yake ya Yanga.

Ngassa alitakiwa kulipa fedha hizo, baada ya kusaini mara mbili Simba na Yanga na kama angeshindwa, basi angefungiwa kucheza soka na kulipishwa faini kutokana na kitendo hicho.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka kwa rafiki wa karibu wa kiungo huyo, Ngassa ameshindwa kucheza katika kiwango chake kutokana na viongozi wa Yanga kumsusia deni la shilingi milioni 45 anazodaiwa na Simba.

Chanzo hicho kilisema kwa makubaliano waliyokubaliana kila mwezi, kiungo huyo alitakiwa kukatwa shilingi 500,000 katika sehemu ya mshahara wake, lakini baadaye mambo yakabadilika akawa anakatwa shilingi 1,000,000.

“Wengi wanahoji kiwango cha Ngassa kimeshuka lakini hawajui sababu, hivi sasa hayupo vizuri, amechanganyikiwa kisaikolojia kutokana na deni analodaiwa kususiwa na Yanga, iliyoamua alipe mwenyewe badala ya klabu kumsaidia kama walivyokubaliana alipotoka Simba.

“Katika makubaliano yao, yeye alitakiwa kukatwa kiasi cha shilingi 500,000 kwa kila mwezi na klabu imuongezee kiasi flani cha fedha kitakachokwenda kwenye deni alilokopa ili ailipe Simba fedha zao walizokuwa wanamdai.

“Kutokana na kiasi hicho cha fedha anachokatwa, anakosa kabisa fedha za matumizi yeye na familia yake kwa kuwa anabakiza kiasi kidogo kwenye mshahara wake.

“Isitoshe hizo fedha zenyewe anazokatwa hazionekani kuongezeka kwenye akaunti hiyo iliyofunguliwa kwa ajili ya kulipia deni hilo la mkopo anaodaiwa, hiyo ndiyo sababu ya msingi Ngassa anashindwa kucheza kwa kujituma ikiwemo kufunga mabao.”

Alipotafutwa Ngassa kuzungumzia hilo alisema: “Hizo taarifa umezipata wapi? Ni kweli kabisa hizo taarifa, kisaikolojia akili yangu haipo vizuri kutokana na deni ninalodaiwa, ukiangalia kiasi cha fedha ninachokatwa kwa kila mwezi ni kikubwa ambacho hatujakubaliana hivyo.

“Tulikubaliana kuwa klabu inisaidie kulipa deni la mkopo niliouchukua ili niwalipe Simba kwa makubaliano ya mimi kukatwa 500,000 lakini ninashangaa imekuwa tofauti, wananikata 1,000,000 katika mshahara wangu.

“Wamenikata kiasi hicho cha fedha kwa mwaka mmoja, sasa wanaponikata kiasi hicho cha fedha mimi ninabaki na kiwango kidogo cha fedha ambacho hakinitoshi kuendesha maisha yangu,” alisema Ngassa ambaye taarifa zinadai analipwa mshahara wa Sh milioni 2.5 kwa mwezi.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top