Unknown Unknown Author
Title: NEWS ALERT: MBUNGE WA ARUMERU MASHARIKI MHE JOSHUA NASSARI AACHIWA KWA DHAMANA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na Woinde shizza, Arusha Hakimu David Mwita wa Mahakama ya mwanzo ya Maji ya Chai mkoani Arusha ameahirisha hadi Desemba 24, 2014 kesi ...
Joshua Nassari
Na Woinde shizza, ArushaHakimu David Mwita wa Mahakama ya mwanzo ya Maji ya Chai mkoani Arusha ameahirisha hadi Desemba 24, 2014 kesi inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Mh. Joshua Nassari (pichani), kwa tuhuma za kuharibu mali ya umma yenye Thamani ya shilingi laki mbili, pamoja na kumteka mtu na kumtishia kwa bunduki tukio ambalo anatuhumiwa kufanya Desemba 15, mwaka huu.

Mahakama hiyo imemuachia Mbunge huyo baada ya kutimiza masharti ya dhamana, ikiwa ni wadhamini watatu ambao wana mali zisizohamishika zenye thamani ya shilingi milioni moja na nusu kila mmoja.

Akiongea mara baada ya kuairisha kesi hiyo wakili wa mbunge huyo wa Arumeru mashariki Bw. James Ole Milya alisema kuwa amesikitishwa sana na tukio la mahakama hiyo kumpa mashariti makubwa mteja wake kwani kesi yake ilikuwa haihitaji mashariti makubwa hivyo. 

Aidha alisema kuwa mbali na kupewa mashariti hayo angependa kesi hiyo ipelekwe katika mahakama ya wilaya ili yeye kama wakili wa mbunge huyo aweze kumtetea kwani katika mahakama ya mwanzo hairuhusu kuweka wakili.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top