Unknown Unknown Author
Title: TRENI YAANGUKA, MABEHEWA YAUNGUA MOTO HUKO PWANI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mabehewa zaidi ya manne ya treni ya mizigo iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar esalaam kwenda Zambia yameteketea baada ya treni hiyo kuanguka ka...
Mabehewa zaidi ya manne ya treni ya mizigo iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar esalaam kwenda Zambia yameteketea baada ya treni hiyo kuanguka katika Kijiji cha Kifulu, mkoani Pwani.
Treni yaanguka
Treni hiyo iliyokuwa na mabehewa 35, ilikuwa ikisafirisha mbolea aina ya sulphur. Kichwa cha treni hiyo kiliacha njia na mabehewa saba kati ya 21 kutumbukia kwenye mtaro.

Wakizungumzia tukio hilo, baadhi ya mashuhuda, Faraji Abduli, Seif Juma Aziza Salimu walisema mabehewa hayo yalianguka jirani na mashamba ya wananchi yaliyokuwa yakisafishwa kwa kuchomwa moto.

Kutokana na moto huo, mabehewa matatu kati ya saba yaliyoanguka, yalishika moto uliosambaa kwenye mabehewa mengine mawili na kuyateketeza.

Hata hivyo, taarifa zilizotufikia baadaye zilidai kuwa kuungua kwa mbolea hiyo kumesababisha madhara kwa baadhi ya wakazi wa eneo la jirani kutokana na moshi kuwaumiza vifua na kusababisha wakohoe.

Kaimu kamanda wa polisi wa Pwani, Mrakibu Mwandamizi SSP Athumani Mwambalaswa alisema:

“Mabehewa 21 yamerudishwa Tazara na taarifa za tukio hilo zitatolewa na Ofisi ya Tazara Dar es Salaam.”

Akizungumzia madhara waliyopata wananchi kutokana na kukohoa kulikosababishwa na moshi huo wa kuungua mbolea, Mwambalaswa alisema wanajitahidi kuwasiliana na wataalamu wa afya ili wafike eneo la tukio.

“Hili la watu kukohoa, siwezi kuthibitisha kwa sasa, maana sisi siyo wataalamu wa afya hadi watakapofika wahusika,” alisema na kuongeza: “Nimewasikia wananchi wakilalamika, lakini mambo yote haya yatazungumzwa na ofisi Tazara na siyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani.”


********************************************
LindiYetu.com ndio mtandao wako kwa habari za burudani, Siasa, Michezo ya Africa na Nje, Tuwe pamoja huku pia >> Instagram Twitter Na Facebook

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top