Unknown Unknown Author
Title: LUIS NANI ANENA HAYA: NINAJITAMBUA KAMA MCHEZAJI WA MAN UTD, NIPO HAPA KUREJESHA KIWANGO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mshambuliaji kutoka nchini Ureno Luís Carlos Almeida Nani, amesema ana hakika bado hajapoteza nafasi ya kuendelea kuitumikia klabu ya Man...
Luis Nani
Mshambuliaji kutoka nchini Ureno Luís Carlos Almeida Nani, amesema ana hakika bado hajapoteza nafasi ya kuendelea kuitumikia klabu ya Man Utd licha ya kupelekwa kwa mkopo kwenye klabu iliyomkuza ya Sporting Lisbon ya nyumbani kwao.

Nani amevieleza vyombo vya habari kwamba kusajiliwa kwa mkopo kwenye klabu ya Sporting Lisbon ni sehemu ya kutaka kumthibitishia meneja wa Man Utd Louis Van Gaal kama ana uwezo wa kuendelea kuwepo kwenye kikosi chake na si kufunguliwa milango ya kuondoka Old Trafford.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, amesema hakuumizwa na kitendo cha kupelekwa kwa mkopo kwenye klabu ya Sporting Lisbon na ndio maana anaitumikia klabu hiyo kwa moyo wake wote.

Amesema anajua mashabiki wengi wanaamini huenda ikawa mwisho wake kucheza soka akiwa na Man Utd, lakini kwake anaamini bado ni mchezaji halali wa klabu hiyo na mwishoni mwa msimu huu atarejea kwa ajili ya kuendeleza mipango ya kuisaidia klabu hiyo iliyomsajili mwaka 2007.

Luis Nani alilazimika kuondolewa kwenye kikosi cha Man Utd mwanzoni mwa mwezi huu na kupelekwa kwa mkopo kwenye klabu ya Sporting Lisbon ya nchini kwao Ureno baada ya kushindwa kumridhisha kiuwezo wa soka meneja wa Man Utd Louis Van Gaal.



********************************************

LindiYetu.com ndio mtandao wako kwa habari za burudani, Siasa, Michezo ya Africa na Nje, Tuwe pamoja huku pia >> Instagram Twitter Na Facebook

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top