BREAKING NEWS: MWANANCHI MMOJA AJERUHIWA KWA KUPIGWA RISASI, KIJIJI CHA MKWAYA - LINDI

raman ya tanzania
Mtu mmoja amejeruhiwa kwa kupigwa risasi katika shamba la Durubay katika kijiji cha Mkwaya Kata ya Mingoyo Mkoani Lindi. Mtu huyo ametambulika kwa jina la laulent Antony ambaye inasadikiwa alikwenda kuokota korosho katika shamba la mwanakijiji ajulikanae kwa jina la Saida, walinzi wawili pia wa eneo hilo wameweza kujeruhiwa kwa mapanga katika miili yao na wananchi wa eneo hlo baada ya kumjeruhi kwa risasi ya moto kijana huyo. Wananchi wa kijiji hcho wamefunga barabara kwa kutumia magogo ya miti ya mikorosho.
ENDELEA KUWA NASI KWA TAARIFA KAMILI.
Na. Ahmeid Abdul Aziz

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post