Unknown Unknown Author
Title: UPDATES:: BARA BARA YA LINDI - DAR ES SALAAM HALI SI SHWARI HIVI SASA. CHEKI PICHA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Barabara kuu iunganishayo mikoa ya Mkoa wa Pwani na Lindi imeharibika Vibaya kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa na Kusabab...
Barabara kuu iunganishayo mikoa ya Mkoa wa Pwani na Lindi imeharibika Vibaya kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa na Kusababisha Adha kubwa ya Usafiri kwa wakazi wa Mikoa ya Lindi na Mtwara wanaotumia Bara bara hiyo kufika Jijini Dar es salaam.

 Eneo Sumbufu kwa muda wote linajulikana na Bado halijafanyiwa matengenezo japo kuwa kuna Mkandarasi aliyepewa Tenda Kutengeneza bara bara hiyo na hivi sasa maeneo mengine tayari yamesha kamilika kwa kuwekwa Lami isipokuwa eneo la Manzese ambalo Ndilo Korofi. 
Viongozi Kadhaa wa Mkoa wa Lindi wameweza Kufika katika eneo la tukio na Kujionea jinsi Abria wanavyopata Bugdha hiyo. 



Abiria inawalazimu kushuka Kwenye Magari yao na Kutembea kwa Miguu kuvuka upande wapili na kutafuta usafiri mwingine ili kuendelea na Safari zao. 
Hakuna Gari linaloweza Kupita katika sehemu hii Hivyo lazima Abiria Washuke na Kukata mbuga ndani ya Tope jingi na kuvuka upande wapili ili kutafuta usafiri mwingine na kuweza kuendelea na safari zao. 


About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top