Unknown Unknown Author
Title: SAMUEL ETO`O AMZABA KIBAO KINGINE JOSE MOURINHO JUU YA UMRI WAKE
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Achana na mimi: Samuel Eto'o alimshambulia kocha wa Chelsea Jose Mourinho baada ya kuambiwa amezeeka. Mapema mwezi huu, Mourinh...
Samuel Eto'o
Achana na mimi: Samuel Eto'o alimshambulia kocha wa Chelsea Jose Mourinho baada ya kuambiwa amezeeka.
Jose Mourinho

Mapema mwezi huu, Mourinho alipachikwa jina la `Mjinga` na Mcameroon, Samuel Eto`o

KWA mara nyingine tena, Mcameroon, Samuel Eto'o ametengeneza vichwa vya habari kwenye magazeti baada ya kumshambulia kocha wa Chelsea Jose Mourinho juu ya umri wake.


Katika mahojiano yake na Tovuti ya shirikisho la Soka la Kiafrika, nyota huyo mwenye miaka 33 amemtaja Mourinho kama `Mnafiki` baada ya awali kumuelezea Mreno huyo kuwa ni `mjinga` .

Kitendo cha Eto`o kuendeleza vita ya maneno na bosi wake kinadhihirisha kuwa Eto`o sasa anaondoka Stamford Bridge.

Eto'o, aliyeshinda taji la UEFA chini ya Mourinho katika klabu ya Inter Milan, aliwaambia cafonline.com:
"Kinyume na maneno ya `mnafiki` juu ya umri wangu, bado niko fiti kiuchezaji".
"Kwa miaka 33, bado najiona kuwa fiti. Nimethibitisha hilo kuwa naweza kufanya vizuri zaidi ya vijana".


Mourinho alinaswa na Camera akisema maneno mabaya kwa Eto`o kuwa umri wa nyota huyo unaweza kuwa zaidi ya umri wake halisi.


Eto'o, ambaye aliifungia Chelsea magoli 12 alishangilia moja ya bao lake kwa staili ya kibabu kinachotembelea mkongojo na kurudia kuwa bado anao uwezo wa kuendelea kucheza ligi za barani Ulaya.
"Napenda kusema kuwa siendi Marekani wala mashariki ya mbali," alisema Eto`o ambaye amemaliza mkataba wake wa mwaka mmoja aliosaini katika klabu ya Chelsea akitokea Anzhi Makhachkala.


"Nitaendelea kucheza `levo` za juu. Nitaendekea kucheza ligi ya mabingwa. Bado nina mapenzi makubwa na mashindano haya".
"Sitawaambieni ni wapi, lakini bado nitakuwa `levo` za juu. Nina miaka 33 na bado nina makombe mawili ya dunia sijacheza".
"kabla yangu mimi kuna wachezaji waliocheza mpaka miaka 41. Kwahiyo namimi naweza"

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top