Unknown Unknown Author
Title: WATU WA TANO WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA KESI YA RUSHWA - LIWALE LINDI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na Mwanja Ibadi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Liwale mkoa wa Lindi imewafikisha mahakamani watu watano k...

Na Mwanja Ibadi
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Liwale mkoa wa Lindi imewafikisha mahakamani watu watano katika kesi mbili tofauti wakiwemo maafisa misitu wawili wa Halmashauri ya wilaya ya Liwale
Hayo yamebainishwa na kamanda wa taasisi ya kupambana na  kuzuia Rushwa wilaya Liwale Asseri Mandari wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juzi
Mandari alisema kati ya tarehe 15 hadi 20  Mwezi Machi 2014. James Nicholaus Kabuta na Nassoro Ally Mzui maafisa misitu wa Halmashauri ya wilaya ya Liwale  na Mtuhumiwa namba tatu Christian Jackob Koka ambaye ni mfanyabiashara mkazi wa Temeke jijijni Dar-es salam wote kwa pamoja wanakabiliwa na kosa la matumizi mabaya ya madaraka kinyume na kifungu namba 31 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa.
Alisema kuwa  Mtuhumiwa namba tatu Christian Jackob Koka mfanyabiashara mkazi wa Temeke jijijni Dar-es  salaam anakabiliwa na makosa mawili; Kosa la kwanza kujipatia manufaa  isivyo halali kinyume na kifungu namba 23(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007  pili  kufanya makosa dhidi ya hifadhi za misitu kinyume na  kifungu cha 84(1)(b) na (5) cha Sheria ya Misitu namba  14 ya mwaka 2002.
Mandari alisema Watuhumiwa namba moja na mbili James Nicholaus Kabuta na Nassoro Ally Mzui maafisa misitu wa Halmashauri ya wilaya ya Liwale walisomewa mashitaka na mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Athuman Burhani mbele ya hakimu wa wilaya ya Liwale  Lilibe M.O. na kukana mashitaka dhidi yake
Aliongeza kuwa kesi nyingine dhidi ya Kaim Salum Mbundi na mwenzake Sadick Kazimoto waanakabiliwa na makosa ya Uchepushaji kinyume na kifungu cha 29 cha Sheria ya Kuzuia  na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.Kughushi kinyume na kifungu cha 333; 335(a)cha Kanuni ya Adhabu na kuisababishia hasara mamlaka kinyume na kifungu cha 57(1) Jedwali la Kwanza aya ya 10 ya Sheria ya Uhujumu Uchumi(CAP 200 R.E 2002).

Mtuhumiwa namba moja Kaim Salum Mbundi ajili ya namba moja alipelekwa katika gereza la Wilaya  Nachingwea baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana  na  kesi namba moja ya  James Nicholaus Kabuta na Nassoro Ally Mzui maafisa misitu wa Halmashauri ya wilaya ya Liwale wanaendelea na dhamana zao na shauri limeahirishwa mpaka tarehe 31/03/2014  wakati juhudi za kumtafuta mtuhumiwa namba tatu zikiendelea

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top