Unknown Unknown Author
Title: VITU 6 VILICHANGIA MOYES KUFANYA VIBAYA MPAKA SASA…!!!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmad Haji Nalaga Kwa heshima na mwendo wa kikaakamavu wima kabisa najitokeza katika blog yenu pendwa wasomaji na kuwapa saluti barabar...

Na. Ahmad Haji Nalaga

Kwa heshima na mwendo wa kikaakamavu wima kabisa najitokeza katika blog yenu pendwa wasomaji na kuwapa saluti barabara na yenye heshima zote.

Nimeamua kijitokeza na kuwa mshiriki wa blog hii (Kuandika) kwa mapenzi yangu, na imani yangu iliyopo kwa timu thabiti iliyopo nyuma ya blog hii. HESHIMA KWENU WOTE, KUANZIA TIMU YA UONGOZI(ADMINISTRATION TEAM), WAPENZI NA HASWA WASOMAJI.

Kwa kuanza leo Nimeandika mada isemayo; VITU VILICHANGIA MOYES KUFANYA VIBAYA MPAKA SASADAVID MOYESKatika moja ya nukuu za JF Kennedy (Anaeaminika kuwa ni mmoja ya wamarekani wenye akili waliowahi kuiongoza Marekani) aliwahi kusema, Mabadiliko ni sheria ya maisha, walewanaoangalia tu yaliyopita na ya sasa wana hakika kuwa watakosa wakati ujao”. Kimsingi kuishi ni kubadilika

Toka kuzaliwa mpaka kufa binaadamu tunapitia mabadiliko mbali mbali, matamu na machungu, yanayoweza kuzuilika na yasiyoweza kuzuilika. Ndio maana hata waliochagua kuwa wahafidhina wameshindwa kudhibiti baadhi ya mabadiliko hata walipokuwa watawala.

Baada ya uongozi wa muda mrefu wa Alex Ferguson katika klabu ya Manchester United ilikuwa ni lazima ingefika siku moja angetoka kwenye kiti hicho kwa namna yeyote ambayo ingesababisha. Wakati ulifika Fergie “Babu” akaondoka na kumteua David Moyes “The Chosen One” kuwa mrithi wake. Hapo ndipo utata wetu unapoanzia.

Mpaka sasa chini ya uongozi wa David Moyes zikiwa zimebakia mechi zisizozidi 6 za ligi, Manchester United hawajachukua wala hawana dalili zozote za kuchukua ubingwa wowote ikiwa ni pamoja na kutokuwa na uhakika wa kupata nafasi ya kushiriki LIGI YA MABINGWA WA ULAYA.

Swali linakuja; Je David Moyes amefeli kumrithi Alex Ferguson katika kuiongoza Manchester United kwenye mafanikio na kulinda ubabe wake? Jibu la mashabiki wengi wa Manchester United ni NDIO ingawa kwangu ni tofauti. Sitaki kusema David Moyes hatofeli kwasababu “kufaulu ni ngumu kuliko kufeli”, ila mpaka sasa hajafeli. Ingawa timu yake haijafanya vizuri

Na hizi ndio sababu zangu

1. Kwanza kabisa ni muda wa mkataba wake

Alipopewa nafasi ya kumrithi Alex ferguusoon alipewa mkataba wa miaka sita, hakupewa timuu kama kocha wa muda kama alivyokachaguliwa Rafael Bennitez au Roberto Di Matteo Chelsea. Hiyo inamaanisha hata malengo/matarajio aliyopewa hayakuua ya muda mfupi. Kuuanzia wamiliki, uongozi mpaka Ferguson mwenyewe waliamini Moyes angehitaji muda kuwapa wanachotaka. Ndio maana hadi leo hamna mtu yeyote toka ndani ya Manchester United amejitokeza na kumkataa Moyes mbele yetu.

2. Presha ya Ferguson kwa wachezajiSIR ALEX FURGUSONUmewahi kufikiria au kufanya kazi chini ya kiongozi unaemwoogopa au/na kumheshimu sana, sanaa? Kama haujawahi wulize waliowahi kuuanya kazi na Mwl. JK Nyerere au wachezaji wa Man utd waliowahi kufanya kazi na Alex Ferguson.

Katika mazingira kama hayo watu huwa watiifu mno, huwa wapiganaji mno, huchapa kazi kwa uwezo wao woote pengine hata kuliko uwezo wao. Nani asiyejua kuuwa Babu alikua baba, babu, kiongozi na mamlaka Old Traford. Hii ilikua aina ya utawwala aliyoitumia Fergie, ilikuwa na matokeo chanya kwa kipindi choote cha uutawala wake. Lakini aina hii ya utawala huwa matokeoo hasi kiongozi huyo anapotoka katika uongozi haswa kama wanaooongozwa waliamini kuwa ni kiongozi wao ndie anaejua nini wafanye, wakati gani na namna gani wafanye ili wafikie mafanikio. Pia huwa hasi kama falsafa yake haikuingia kwenye vichwa na mioyo ya waongozwa.

Wachezaji wa Manchester wamechoka kwa sababu wengi wao walijituma sana, walifanya kazi kubwa kupigania timu ya Alex Ferguson, wengine juu ya uwezo wao. Katika hali ya kawaida nani angempa namba katika kikosi cha kuanza cha timu kubwa nne za ligi kuu England wachezaji kama Chris Smallin, Phil Jonnes, Carrick au Cleverly? Ikiwa wachezaji kama Mikel Obi, Demba Ba, Torres, David Luis,Thomas Rosicky, Edin dzeko, Vermalain hawana uhakika wa namba katika timu zao? Au nani angemsajili Antonio Valencia kama mtu wa kuziba pengo la Christiano Ronaldo? Hawa woooote walijituma mno wakati wa Fergie kwa uwezo wao wote au/na wengine hata zaidi ya uwezo wao na sasa aidha wamechoka au hawaihisi tena ile presha iliyokuwa ikiwasukuma, pengine wanakabiliwa na yote.

3. Wachezaji wazeerio vidic evraZaidi ya wachezaji sita wanounda uti wa mgogo wa timu aliyoachiwa David Moyes wana umri uliozidi umri wa kawaida wa kucheza soka la ushindani. Nemanja Vidic 32, Rio Ferdinand 35, Patrice Evra 32, Michael Carrick 32, Ryan Giggs 40, Robin Van Persie 30 (ambae ukichukulia na rekodi yake ya majeruhi ni kama ana miaka 33, ni kama ana miaka miwili tu ya soka la ushindani) huku ukimuacha nje Darren Fletcher 30 ambaye ni kama alitolewa kwenye kikosi cha kwanza. clip_image002Ukiondoa swala la “Huwezi kumfundisha mbwa mzee mbinu mpya” kama waingereza mwenyewe wanavyosema, wachezaji hawa ambao ndio walikua uti wa mgongo wa timu wanakuwa sio sehemu ya falsafa ya kocha mpya.gigs fletcherHili limepelekea Moyes kujaribu wachezaji wengi katika msimu kabla ya kupata timu yake, lakini pia limepunguza morali ya wachezaji wakongwe kwasababu wanajiona sio sehemu ya mipango ya kocha mpya. Na huo ndio ukweli, katikati ya msimu tushaanza kuskia Evra, Vidic, Ferdinand wataondoka. Giggs atastahafu. Hii si sawa, ilitakiwa itokee mwishoni mwa msimu haswa ukizingatia kuwa wachezaji hawa hawastahafu ila wanahama timu. Wote tunakumbuka msimu uliopita siku ambayo Aaron Ramsey alipiga goli mbili za kufungia msimu tukaskia Michael Owen, Paul Scholes, David Beckham, Jimmie Carrragher na Petrov walitangaza kustaafu soka. Katika mahusiano mazuri na klabu na kwa faida ya morali ya timu hutegemei mchezaji au wechezaji haswa wakongwe wa timu kutangaza kuhama timu katikati mwa msimu. Hapa wazee wamemyumbisha “The chosen One na kikosi chake”

4. Mbinu mpya

Katika hili nadhani David Moyes alienda mbio sana bila kujali mfumo uliomtangulia uliwa na mizizi mirefu kiasi gani.

Kwa mfano “The Chosen one”aliondoa benchi lote la ufundi lilikuwepo kabla ya ujio wake, alikuja na mbinu mpya za ufundishaji,mbinu mpya za mazoezi (ambazo mara kadhaa tumeskia Robin Van Persie akizilalamikia).

Haya yote ukichanganya na mtindo mpya wa uchezaji ni wazi moyes aliitaji muda zaidi kufika mafanikio, na Moyes asingeyafanya yote haya kama angejua amepewa miezi 6. Angetembea katika nyayo za Fergie tu kama ambavyo Avram Grant na Roberto Di Matteo walivyowahi kufanya Chelsea walipopewa timu kwa muda wakiwarithi watangulizi wao.

5. Msingi wa timu

Ili kuwa na timu imara na utawala madhubuti katika timu au uongozi wowote lazima uwe na msingi wako katika oganazesheni husika. Lazima uwe na watu/waajiriwa wanokuelewa vyema na ambao wanaielewa, kuiamini na kuifuata barabara falsafa yako.mourinhoMourihno pale Chelsea ana JohnTerry, Frank Lampard, Petr Cech, Ramires, Oscar, Hazard. Marcio Maximo alikuwa na Nizar Khalfan, Nadir Haroub, Shaban Nditi. Wenger ana Per Mertesacker, Laurent Koscienly, Jack Wilshere, Aaron Ramsey, Theo Walcot.

Umuhimu wa wacheza ambao ni msingi/uti wa mgongo wa timu ni kuwa na wachezaji ambao wapo kwenye timu wakati wote, wanatengenezwa kuilewa, kuikamilisha na kuiongoza falsafa ya mwalimu. Pia hawa ndio msingi wa kujenga timu ya muda mrefu.

Kimsingi toka msimu uliopita Man Utd ilionekana kama haina wachezaji ambao ni msingi wa timu. Ikiwa Wayne Rooney ambae alikuwa katika umri na kiwango sahihi hakumuhakikishia “The Chosen one” kuwepo katika mipango ya muda mrefu. Nani katika kiwango kipi kipindi Moyes anachukua timu angeweza kuwa katika msingi wa timu?

Taratibu Moyes ameanza kujenga msingi wa timu. Wayne Rooney baada ya mvutano wa muda mrefu sana amesaini mkataba mpya wa muda mrefu (miaka mine), Juan Marta katika umri na kiwango kizuri kabisa anaingia moja kwa moja, kuna Fellaini, Adnan Januzaj. Tumpe muda alifanye hili vizuri

6. David Moyes “The Chosen One” hatishi

Kutokana na ukweli kuwa anatoka katika timu isiyo na heshima/nafasi ya juu na yeye mwenyewe kuonekana hivyo inawapa moyo/imani ya timu nyengine kupambana kwa nguvu zote wakiamini timu ya David Moyes inafungika.

Waswahili tunasema, “Imani inaponya”. Kuna timu nyingi ambazo zimepata matokeo chanya dhidi ya Man Utd kwasabu ya imani ya kupata matokeo chanya zaidi. Hii pia ilitokana na ukweli kuwa hata wachezaji wa Man Utd wenyewe kuna kipindi wanapoteza ule upambanaji waliokuwa nao wanapojua nyuma yao kuna “Babu”.

Kama hivyo ndivyo, basi lazima tukubaliane kuwa kadri dunia inavyolizunguka jua na kufanya miaka na majira yake na mambo yanabadilika na Ferguson muda wake kuondoka Man Utd ulifika. Na kama alivyowahi kusema JF Kennedy kuwa, Mabadiliko ni sheria ya maisha, walewanaoangalia tu yaliyopita na ya sasa wana hakika kuwa watakosa wakati ujao”. Basi yatupasa kukubali kuwa huu ni wakati wa “The Chosen One”, hajafeli kama wengi waaminivyo na ataipeleka Man. Utd kule alikoagizwa aipeleke. Tumpe muda

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top