Unknown Unknown Author
Title: UCL: MAN UNITED YAMSIMAMISHA BINGWA BAYERN…!! KWA DROO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
MABINGWA wa Ulaya, Bayern Munich, Usiku huu wamepata Sare ya Bao 1-1 walipocheza Uwanjani Old Trafford na Mabingwa wa England Man United kat...

clip_image001[5]MABINGWA wa Ulaya, Bayern Munich, Usiku huu wamepata Sare ya Bao 1-1 walipocheza Uwanjani Old Trafford na Mabingwa wa England Man United katika Mechi ya Kwanza ya Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na Bayern kumaliza Mtu 10 baada ya Kiungo wao mahiri, Bastian Schweinsteiger, kutolewa kwa Kadi Nyekundu kufuatia Kadi za Njano mbili.clip_image001Bayern walimiliki sana Mpira katika Kipindi cha Kwanza lakini ni Man United ndio waliokosa nafasi ya wazi wakati Danny Welbeck alipobaki yeye na Kipa Neuer na kujaribu kufunga kiufundi lakini Kipa huyo wa Germany akaokoa Bao la wazi.clip_image001[11]Mapema kwenye Dakika ya 3, Welbeck alifanikiwa kufunga Bao safi lakini Refa Carlos Velasco Carballo kutoka Spain alilikataa na kuwaacha Wachambuzi wengi kukuna vichwa vyao kwanini Bao hilo lilikataliwa.

Hadi Mapumziko Mechi hii ilikuwa 0-0.

VIDIC GOALKipindi cha Pili, Dakika ya 58, Man United walifunga Bao kwa Kichwa cha Nahodha wao Nemanja Vidic baada kuunganisha Kona ya Wayne Rooney.

Bayern walisawazisha katika Dakika ya 66 baada ya Krosi ya kumkuta Mario Mandzukic aliemsogezea Bastian Schweinsteiger na kufunga.clip_image001Katika Mechi ya Marudiano, mbali ya kumkosa Bastian Schweinsteiger pia itamkosa Javi Martinez baada Mchezaji huyo kuzoa Kadi ya Njano ambayo itamfanya akose Mechi ya Marudiano.

Timu hizi zitarudiana huko Allianz Arena Jijini Munich hapo Jumatano Aprili 9.

VIKOSI:MANCHESTER UNITED: De Gea; Jones, Ferdinand, Vidic, Büttner; Valencia, Carrick, Fellaini, Giggs, Welbeck; Rooney

Akiba: Lindegaard, Hernandez, Nani, Young, Fletcher, Januzaj, Kagawa.

BAYERN MUNICH: Neuer; Rafinha, Boateng, Martinez, Alaba; Lahm; Robben, Kroos, Schweinsteiger, Ribéry; Muller

Akiba: Starke, Van Buyten, Mandzukic, Shaqiri, Pizarro, Gotze, Hojbjerg.

REFA: Carlos Velasco Carballo (Spain).

 

Marudiano[Saa 3 Dak 45 Usiku]

Bayern Munich v Manchester United [1-1]

Atletico Madrid v Barcelona [1-1]

 

MECHI ZA KESHO NI: Jumatano Aprili 2

Real Madrid v Borussia Dortmund

Paris Saint-Germain v Chelsea

 

UEFA CHAMPIONZ LIGI: WAFUNGAJI BORA 2013/14:

C. Ronaldo-Real Madrid Goli 13

Zlatan Ibrahimovic-PSG Goli 10 [Penati 1]

Messi-Barcelona Goli 8 [Penati 2]

Diego Costa-Atletico Madrid Goli 7

Sergio Agüero-Manchester City Goli 6 [Penati 2]

WASHINDI [Miaka ya karibu]:

MSIMU

MSHINDI

NCHI

MSHINDI WA PILI

NCHI

GOLI

2012-13

Bayern Munich

Germany

Borussia Dortmund

Germany

2-1

2011-12

Chelsea

England

Bayern Munich

Germany

1-1 (4–3)

2010-11

Barcelona

Spain

Manchester United

England

3-1

2009-10

Internazionale

Italy

Bayern Munich

Germany

2-0

2008-09

Barcelona

Spain

Manchester United

England

2-0

2007-08

Man United

England

Chelsea

England

1-1 (6–5)

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top