Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda boti kutoka mkoa wa Kigoma kuelekea Karema mkoani Katavi kwa siku nne.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi wa kijiji cha Sigunga wilayani Uvinza mkoani Kigoma alipowasili kijijini hapo kuzungumza wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi,wengine wanaonekana kwenye picha ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Balozi Ali Abeid Karume.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiondoka kijijini Sigunga baada ya kuzungumza wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi,wengine wanaonekana kwenye picha ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi anayepiga kasia na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Balozi Ali Abeid Karume.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitembea kwenye mitaa ya kijiji cha Mgombo Kata ya Buhingu wakati aliposimama kuwasalimia wanakijiji hao,Kinana ni Katibu Mkuu wa kwanza wa CCM kufika kijiji cha Buhingu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapungia mkono wakazi wa Karema mara baada ya kuwasili katika bandari ya Karema mkoani Katavi.
Umati wa watu uliofika kumlaki Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na msafara wake walipowasili Karema mkoani Katavi
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.