REAL MADRID NA BAYERN MUNICH ZINAKUTANA LEO KWENYE KOMBE LA UEFA


Cristiano Ronaldo anatarajia kurudia dimbali kuitumikia Real Madrid leo kwenye mchezo wa awali wa nusu fainali ya Champions League dhidi ya Bayern Munich katika uwanja wa Santiago Bernabeu.
Kocha wa Madrid Carlo Ancelotti amesema atafanya maamuzi juu ya mchezaji huyo mwenye miaka 29 ambaye alikosa michezo minne ya mwisho ya klabu hiyo ukiwepo mchezo wa fainali ya Kombe la Mfalme ambapo Madrid waliishinda Barcelona 2-1.
Pep Guardiola, próximo entrenador del Bayern Munich, descartó el ...Naye Boss wa Bayern Munich Pep Guardiola hajawahi kupoteza hata mchezo mmoja katika michezo sita aliyocheza na Real Madrid katika dimba la Bernabeu.
Bayern Munich imeichapa Real Madrid mara nne katika michezo mitano ya nusu fainali ya European Cup ambapo timu hizo zimekutana.

Real inajivunia rekodi yao ya kutwaa taji la Champions League mara tisa lakini inalisaka taji hilo kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 12.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post