Ludovick Mwananzila Mkuu wa Mkoa wa Lindi
(picha na Maktaba)
Na. Mwanja Ibadi..Lindi
Mkuu wa mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila amewataka Wadau elimu
mkoani humo kutambua umuhimu wa elimu kwa kuwapeleka
watoto wao shuleni ili waweze kupata haki yao ya msingi ya kupata elimu ambapo
itawasaidia kuweza kuwa na maisha bora ya baadaye.
Agizo hilo
amelitoa kwenye kikao cha wadau elimu mkoa wa Lindi
kilichofanyika kwenye ukumbi wa Kagwa jana.
Mwananzila
alisema Moja ya haki za watoto wanazotakiwa kupewa ambazo zimeainishwa katika
sera na mipango mbalimbali ya serikali ni kupata haki ya elimu kwa kuwa elimu ni
ufunguo wa maisha na rasilimali pekee ambayo itaweza kumfanya aweze kuwa na
uhakika wa kuweza kujitegemea katika maisha yake ya baadaye.
Alisema iwapo mzazi ama mlezi atashindwa
kumpeleka mtoto wake shuleni kwa sababu ambazo si za kimsingi hatakuwa anamnyima
haki ya kupata elimu na kwamba uwezekano wa mtoto kuwa na maisha yasiyo na
uhakika ni mkubwa na kwamba taifa litakuwa na kizazi kisichokuwa na
uwelewa.
“Kwa maisha ya
sasa niwakumbushe wazazi na walezi kuwa hakuna rasilimali kubwa kwa mtoto
anayotakiwa kupewa isipokuwa elimu…elimu ndio rasilimali ambayo mtoto anatakiwa
kurithishwa na mzazi hivyo wazazi tuzingatie umuhimu wa kuwapatia elimu watoto
wetu ili waweze kujikomboa kimaisha ya baadaye,”alisema Mwananzila
Mwanazila alisema
kuwa changamoto kubwa iliyopo katika jamii ni kwamba uwelewa mdogo
kuhusu umuhimu wa elimu hali inayochangia baadhi ya wazazi na walezi kushindwa
kuwapelaka watoto wao shuleni lakini kupitia elimu wanayoitoa imesaidia kuifanya
jamii kuanza kuwa na mwamko wa kuzingitia suala la elimu.
Alisema kwa
kulitambua ili mkoa umepanga mikakati mbalimbali ikiwemo ya kufanya vikao kwa
kujadili changamoto hizo kwa kuzitafutia majibu
Awali katibu
tawala mkoa wa Lindi Abdala chikota aliwataka wadau hao kutambua
kuwa wajibu kusimamia na kutekeleza majukumu ya maendeleo ya mkoa
yatafanywa na wadau wanaopenda maendeleo katika mkoa huyo.
Chikota Alisema
kushuka au kupanda kwa kiwango cha taalumu kunategemea kuwajibika kwa wadau
kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto na kutengeneza miundombinu
rafiki kwa watendaji wakiwemo walimu.
Tags
HABARI ZA KITAIFA