Unknown Unknown Author
Title: CCM YASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Ridhiwani Kikwete akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupiga kura mjini Chalinze jana.. Ridhiwani Kikwete aliyekuwa mgombea ubunge ...

clip_image001Ridhiwani Kikwete akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupiga kura mjini Chalinze jana..

Ridhiwani Kikwete aliyekuwa mgombea ubunge uchaguzi mdogo jimbo la chalinze bagamoyo mkoani pwani kupitia chama cha mapinduzi CCM ,ameibuka kidedea kwa asilimia 86.61 katika uchaguzi huo na kuwamwaga wagombea wengine kutoka vyama vinne vya upinzani.

Matokeo ya uchaguzi huo yanaonyesha Ridhiwani ameongoza akifuatiwa na CHADEMA ,CUF,NRA na ASP.

Matokeo hayo yametangazwa usiku wa kuamkia leo April 7 majira ya saa nane usiku katika shule ya sekondari Chalinze na  Msimamizi wa uchaguzi huo  Bw.Samwel Salianga ambapo amesema CCM –Ridhiwani Kikwete amepata kura  20,828 sawa na  86.61%,Chadema-Mathayo Torongei amepata kura 2,544 sawa na asilimia 10.58,CUF- Fabian Skauki  476 sawa na asilimia 1.98,NRA-Hussein Ramadhani kura 60 asilimia 0.25 huku AFP Ramadhani Mgaya amepata kura 186 sawa na asilimia 0.59.

Salianga amesema kati ya watu waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ni watu elfu 92,waliojitokeza katika zoezi hilo ni watu 24,422 ambapo kura halali zilikuwa 24,047 na  kura 375 zikiharibika.

Wagombea waliokuwepo wakati wa kutangaza  matokeo katika uchaguzi huo na kusaini fomu ya kukubalina na matokea alikuwepo mgombea wa NRA na CCM pekee.

Aidha Wakizungumza baada ya kupokea matokeo hayo aliyekuwa mgombea wa chama cha NRA pamoja na Ridhiwani Kikwete kupitia CCM,kila Mmoja ameshukuru wananchi na kuahidi kushirikina na wananchalinze kuleta maendeleo.

>>MichuziJr blog

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top