MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga, Wameyaaga Mashindano ya Afrika ya CAF CHAMPIONZ LIGI baada kutolewa na Mabingwa Watetezi wa Afrika, Al Ahly, kwa Penati 4-3.
Kwenye Mechi ya Usiku Hapo jana iliyochezwa bila Watazamaji ndani ya Uwanja Harras El-Hedoud Mjini Alexandria, Nchini Misri, Al Ahly walishinda Bao 1-0, kwa Bao la Dakika ya 71 la Sayed Moawad, na hivyo kuipeleka Mechi kwenye Tombola ya Penati kwa vile Yanga walishinda Mechi ya Kwanza Jijini Dar es Salaama Bao 1-0.
Penati za Yanga zilifungwa na Didier Kavumbagu, Nadir Haroub ‘Canavaro’, Emmanuel Okwi na waliokosa ni Oscar, Said Bahanuzi na Mbuyu Twite huku pia Kipa Deo Munish akiokoa Penati mbili.
Matokeo haya yameiacha Tanzania bila Klabu yeyote kwenye Michuano ya Afrika baada ya Klabu 3, Azam FC, KMKM na Chuoni, kutolewa nje Raundi iliyopita kwenye CAF CHAMPIONZ LIGI NA Kombe la Shirikisho.
Sasa Al Ahly wanatinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na watacheza na Al Ahli - Benghazi ya Libya.
VIKOSI: ALA AHLY: Sherif Ekramy, Saad Samir, Mohamed Naguib, Ahmed Fathi, Sayed Moawad, Rami Rabia, Hossam Ashour,Abdallah El-Said, Moussa Yedan, Gedo, Amr Gamal
YANGA: Deo Munish "Dida", Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub "Cannavaro", Kelvin Yondani "Cotton" , Frank Domayo "Chumvi", Saimon Msuva, Mrisho Ngasa, Didier Kavumbagu, Emmanuel Okwi, Hamisi Kizza
Akiba: Kaseja, Juma, Luhende, Athuman Iddi "Chuji", Nizar Halfan, Said Bahanuzi , Jerry Tegete
Refa: Badara Diatta [Senegal]
TAZAMA VIDEO HAPA::
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.