CANNAVARO AONYWA NA BUSHIRI

clip_image001BAADA kuonyesha uwezo wa juu katika mechi mbili za kimataifa alizocheza dhidi ya Al Ahly ya Misri, beki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, ametakiwa kuhakikisha analinda kiwango chake hicho ili kisiporomoke kama ilivyokuwa hivi karibuni.

Kocha Mkuu wa KMKM inayoshiriki Ligi Kuu Zanzibar, Ally Bushiri, alisema Ijumaa kuwa Cannavaro anatakiwa kuhakikisha analinda kiwango chake hicho cha sasa ili aondokane na kelele za mashabiki wa Yanga zilizokuwa zikimwandama hapo awali.

Bushiri ameongeza kuwa hali hiyo itamsaidia kujitengenezea mazingira mazuri ya kumaliza soka lake kwa heshima kubwa na mafanikio ya hali ya juu.

“Tumesikia kuwa Al Ahly baada ya mechi yao ya marudiano wameonyesha nia ya kumhitaji Cannavaro pamoja wachezaji wenzake wawili. Hiyo ni moja ya mafanikio makubwa kwake, anatakiwa kulinda kiwango chake kwa faida yake, Taifa Stars na Zanzibar Heroes,” alisema Bushiri.

Kabla ya Yanga kupambana na Al Ahly, Cannavaro alikuwa katika wakati mgumu kutoka kwa mashabiki wa Yanga ambao walikuwa wakimzomea kila wakati kutokana na kuporomoka kwa kiwango chake

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post