Kuanzishwa kwa juhudi mpya za utafutaji wa ndege katika Bahari ya Hindi huenda kukatoa sura mpya ya matumaini hasa kutokana na ripoti kuwa huenda ndege hiyo ilibadilisha mwelekeo wa safari.Napoli. Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Italia Mario Balloteli ameelezea kukerwa na kitendo cha Afisa Mkuu wa Mamlaka za usafiri wa Anga ya Malaysia Azharuddin Abdul Rahman kumfananisha na abiria wawili wanaodaiwa kutumia hati bandia za kusafiria kwenye ndege iliyopotea ya Malaysia.
Hivi karibuni wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusiana na watu wanaodaiwa kutumia hati bandia kwenye ndege iliyopotea, Rahman alisema kuwa watu hao walikuwa wamefanana kwa sura na mchezaji huyo wa AC Milan.
Ofisa huyo alifafanua kuwa “abiria waliotumia hati bandia za kusafiria na kisha kuingia kwenye ndege hiyo aina ya MH370 ya Shirika la Ndege Malaysia wanafanana na Balotelli.”
Balotteli anadaiwa kusema ni jambo la kuudhi kuona Bw Rahma akimfananisha na wahalifu licha ya kutokuwa na abiria mweusi katika ndege hiyo.
Balloteli ambaye ni mmoja ya wachezaji wanaotajwa kuwa na vituko zaidi uwanjani amemtaka ofisa huyo kuomba radhi haraka iwezekanavyo.
Msako wa ndege sasa wahamia Bahari ya Hindi
Kumekuwa na juhudi kubwa za kuisaka ndege hiyo ambayo inasadikiwa huenda ikawa imeanguka baharini kutokana na mazingira ya kutatanisha yanayohusishwa na tukio la kupotea kwake.
Maofisa wa Marekani ambao wameunga mkono msako huo wamekwenda mbali zaidi kwa kuihusisha bahari ya Hindi na wametuma meli moja inayozunguka eneo hilo kwa matarajio kuwa huenda ndege hiyo imebadilisha mwelekeo.
Afisa wa jeshi la majini la Marekani ameliambia shirika la habari la AFP kwamba meli ya jeshi hilo, USS Kidd, inaelekea katika bahari ya Hindi kusaidia kuitafuta ndege hiyo aina ya Boeing 777 iliyotoweka ikiwa njiani kuelekea Beijing ikitokea Kuala Lumpur ikiwa na watu 239.
CHANZO: MWANANCHI
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.