HII INAWAHUSU MASHABIKI WA MAN UNITED, FEB 6TH 1958 MUNICH FOREVER REMBERED

Tarehe kama ya leo mwaka 1958 yaani ( 6 February 1958)
Timu ya soka Manchester united ikiwa na kikosi chenye vijana wastani wa miaka 24 kinachoaminika Kuwa imara kuwahi tokea katika historia ya klabu hiyo chini ya kocha matt busby na kupewa jina la "Busby Babes" kilikuwa kinasafiri kutoka Yugoslavia ambapo walitoka kucheza dhidi ya Red star Belgrade ya nchini humo katika kombe la ulaya yaani " European Cup"clip_image002
Ilipofika ujerumani katika uwanja wa Munich Riem Airport ilibidi watue ili ndege iongezewe mafuta!baada ya hapo katika jaribio la Tatu kupaa ndege hiyo ikagonga baadhi ya majengo ikaanguka na kuanza kuwaka moto!

Ndani ya msafara huo kulikuwa na jumla ya watu 44, kati yao kulikuwa na wachezaji, maofisa wa timu, waandishi wa habari na mashabiki ambapo watu 20 hapo hapo walipoteza maisha huku wengine wakikimbizwa katika hospitali ya Recht der Isar ya jijini Munich ambapo dakika chache watu 3 walikufa na kufanya idadi ya waliokufa Kuwa 23 na 21 walinusurika huku kocha mkuu Matt Busby akiwa mahututi na kapteni ambaye hadi leo huwa anaonekana katika mechi za man utd Bobby chalton akinusurika salmini! wachezaji 8 walikufa hapo happo na maofisa 3 wa timu!

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post