Mh. Khalfani Barwany Mb jimbo la Lindi akiongea na waandishi wa Habari. (Hawapo pichani, Picha na Maktaba)
Lindiyetu.com baada ya Kupata taarifa za Chama cha Wananchi C.U.F kumvua uanachama ndg Abdallah Khatau aliyekuwa diwani wa Kata ya makonde Manispaa ya Lindi kwa Kosa la UTOVU WA NIDHAMU ANAOUONYESHA NDANI YA CHAMA HICHO uliamua kutafuta ukweli wa hilo lililokuwa likisemwa na baadhi ya wananchi wa Manispaa hii.
Minongono hiyo ilianza hapo jana katika mkutano wa Mh. Mbunge alioufanya katika Manispaa hiyo ya Lindi.
Lindiyetu.com iliweza kuongea na Mh. Mbunge wa Jimbo la Lindi na kusema ni kweli ndg Abdallah Khatau amevuliwa uanachama wa chama cha Wananchi C.U.F kupitia kikoa cha kamati tendaji cha Manispaa ya Lindi ya Chama Hicho na Kufikia uamuzi wa Kumvua uanachama Diwani huyo wa Kata ya makonde,
Hata hivyo aliongeza kuwa Chama Hicho kimetoa Onyokali kwa Diwani wa Mitandi Ndg Hafidhi Chitutu Baada ya Kuomba radhi chama hicho kwa kile kile kinachosemwa ni Utovu wa Nidhamu.
Hayo yamethibitishwa na Mbunge wa jimbo la Lindi Mh. Salum Khalfan Barwany, alipoongea na Lindiyetu.com
Chama hicho kinajiandaa kuwasilisha taarifa rasmi kwa Mkurungezi wa Manispaa ya Lindi ya Kuwa nafasi ikowazi katika kata hiyo hivyo yawezekana uchaguzi mdogo kufanyika hivi karibuni.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.