BILL GATES AMEJIONDOA UENYEKITI WA MICROSOFT, HUYU NDIO CEO MPYA

Mmiliki wa Microsoft  Bill Gates amejiondoa kama mwenyekiti wa kampuni yake ya Microsoft na kushika wadhifa mpya kama mshauri wa teknolojia. Satya Nadella ametajwa kuwa mwenyekiti mtendaji mkuu wa kampuni hiyo.clip_image002Tangazo la CEO mpya limekuja baada ya aliyekuwepo Steve Ballmer kutangaza mwaka jana nia yake ya kustafu.

Nadella anakuwa mwenyekiti mtendaji wa tatu katika historia ya miaka 39 ya Microsoft, baada ya mwanzilishi mwenza Bill Gates na Steve Ballmer.

Microsoft imesema John Thompson atachukua nafasi ya uenyekiti iliyoachwa na Bill Gates.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post