Kuna mambo matatu ya msingi sana ya kufanya kila unapo amka Asubuhi yataifanya siku yako kuwa ya mafanikio sana.
1. Kufanya mazoezi ya viungo. Ni muhimu sana kufanya mazoezi hasa wakati wa asubuhi maana mazoezi huchangamsha akili na kukuwezesha kufikiri kwa ufasaha zaidi. Pia mazoezi yanaimarisha afya na afya njema ni muhimu sana kwako kufikia malengo yako.
2. Kupitia malengo na mipango ya siku. Katika muda huu wa asubuhi pitia malengo uliyojiwekea maishani na mipango mbalimbali ya kufikia malengo hayo. Pia weka mipango ya siku hiyo na jinsi ya kuitekeleza. Katika saa hii unaweza kuangalia ni kwa kiasi gani umefanikiwa ama umekaribia kuyafikia malengo yako.
3. Kujihamasisha. Ni muhimu sana kujihamasisha kabla hujianza siku yako. Hii itakusaidia kuweza kuimiliki siku yako na kuwa na mtizamo chanya juu ya maisha yako na kazi zako. Unaweza kujihamasisha kwa kujisomea kitabu, kusikiliza vitabu vilivyosomwa au kuangalia video mbalimbali za kuhamasisha.