Msanii wa Kenya Jaguar ametoa wimbo mpya ‘Kioo’ pamoja na video yake ambayo alishoot katika moja ya magereza ya Kenya (Industrial Area prison).‘Kioo’ ni wimbo ambao Jaguar anazungumzia safari yake ya maisha na jinsi ambavyo hujitazama mara kwa mara katika kioo kuona kiasi gani amepiga hatua.
‘Maisha ni kama safari, hakuna ajuaye kesho itakuwaje’ ni maneno yanayosikika mwanzoni mwa wimbo huo.
Baadhi ya shots za video hii zilichukuliwa gerezani akiwa na baadhi ya wafungwa kabisa sio wa kuigiza, ambao alijichanganya nao akiwa kama mfungwa ambaye baadaye alikuja kuachiwa huru ikiwa ni sehemu ya ujumbe wa safari yake ya maisha katika wimbo huo.
Itazame hapa:
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.