Shettta ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa tayari ameshafanya ngoma nyingine na Diamond Platinumz inayoitwa Mama Qayllah na umetayarishwa na Shedy Clever wa Burn Records.
“Kwanza kabla ya yote ningependa kutoa shukrani za dhati kwa mashabiki wangu kwa kuipokea vizuri video ya wimbo wangu 'Sina Imani', kwa sasa nipo katika maandalizi ya wimbo wangu mwingine mpya kabisa humo ndani nipo mimi pamoja na Diamond,wimbo unaitwa Mama Qayllah.
Bado upo katika hatua za mwisho za kufanyiwa mixing na Sheddy Clever wa Burn Records.” Amesema Shetta.
Shetta ama Baba Qayllah kama anavyopendwa kuitwa amesema huo utakuwa wimbo wake wa mwisho wa kufungia mwaka 2013.
Source-Times Fm
Tags
HABARI ZA WASANII