MISS TANZANIA 2012 BRIGITTE ALFRED AONDOKA LEO KWENDA KAMBI YA MISS WORLD INDNESIA

clip_image001Mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Urembo ya Dunia, Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred Lymo, ameondoka nchini leo kwenda nchini Indosia katika kambi ya Miss World 2013. Pichani juu ni Brigitte akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam jioni hii tayari kwa safari hiyo.

Akiongea na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuondoka nchini akiwa uwanjani hapo Brigitte ameahidi kufanya vyema katika mashindano hayo huku akiwaomba watanzania kumpa suport kwa kumpigia kura pindi zoezi hilo liytakapo anza kupitia tovuti ya Miss World.Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, kupitia kampuni ya Lino International Agency, Hashim Lundenga akimwelekeza machache mrembo huyo kabla ya kuondoka.Lundenga akizungumza huku Miss Tanzania 2013, Brigitte Alfed na mama yake wakisikiliza.Baadhi ya viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na mrembo huyo uwanja wa Ndege hii leo.Mama na Mwana....Miss Tanzania akilamba picha na mama yake kabla ya kuruka kwenda Indonesia hii leo. 

SOURCE: FATHER KIDEVU BLOG

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post