ANGALIA PICHA ZA MAZISHI YA ASKOFU KULOLA HAPO JIJINI MWANZA.

clip_image001Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo akiongoza wanachi kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Askofu wa EAGT Moses, Kulola

Mchungaji Kadani Limbu ambaye ni Katibu wa Kanisa la EAGT Makao Makuu (Ujenzi) akisoma wasifu wa marehemu Askofu Kulola aliyezaliwa 1928 katika Kijiji cha Nyang’honge Wilayani Kwimba Mkoani Mwanza na kujaliwa kupata elimu ya msingi (Middle School) na sekondari ya Bwiru Boys Mwanza kati ya mwaka 1946 hadi 1949 kuendelea na masomo na kupata Civil Technician.

Baada ya kumaliza na kupata utaalamu huo na kuajiliwa kuwa mtumishi wa serikali katika Halmashauri ya Mji wa Mwanza kama Mhandisi wa Mchoraji wa Ramani za majengo na Barabara wakati wa uhai wake aliamua kuacha kazi na kuanza utumishi wa mungu akifanya kazi kwa kutembea kila mahali akihubiri Injili kwa watu mbalimbali.

Wasifu huo ulimwelezea Askofu Kulola wakati wa utumishi wake wa kiroho kuwa  alikuwa akitembea kwa miguu kuanzia mwaka 1962 akihubiri neno la Mungu .Baada ya kuacha kazi za serikali mwaka 1951 alipatwa na matatizo na kuwahi kufungwa gerezani na kupigwa na bwana jela na kuumizwa vibaya muguu wake wa kushoto na kupelekea kupata kilema ambapo aliwekewa mguu wa bandia.

Marehemu Askofu Kulola ameacha mke na watoto 10 wajukuu 42 vitukuu 16 na amekuwa mutumishi wa kiroho tangu  akiwa na umri wa miaka 18 ....

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post