YAHAYA MUSIC VIDEO KUONYESHWA IJUMAA YA TAR 16 AUGUST 2013 - NYUMBANI LOUNGE

clip_image001Kwanza kabisa poleni sana kwa kusubiri muda mrefu.
Kutokana na marekebisho ya hapa na pale ndio maana video ya YAHAYA ikachelewa kutoka

Hivi sasa iko tayari, tumeona si vibaya tukaifanyia kiji party kidogo cha utambulisho
Kikiambatana na BBQ, na Shooters za hapa na pale kuupendezesha usiku wako.

Party ya kuitambulisha Video ya Yahaya, ambayo imefanywa na Ogopa DeeJays
Itaanza saa 4:00usiku (10:00pm) ikiambatana na burudani ya muziki toka kwa JayDee na Machozi Band

Baada ya hapo video itagaiwa kwa televisheni zote ili walio mbali, ambao hawakuweza kuhudhuria nao wapate kufaidi uhondo huo.

Karibuni sana siku hiyo ya Ijumaa tar 16 August, pale Nyumbani Lounge

Imetolewa na Lady Jaydee

Ladyjadee.blogspot.com

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post