Unknown Unknown Author
Title: WAKULIMA WAKOROSHO WATAKIWA KUJITAMBUA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Waziri wa Kilimo, chakula na ushirika Mhandisi Christopher Chiza Na Abdulaziz Video,Dodoma WAKULIMA wa zao la korosho nchini wametakiwa kub...

UFUNGUZIWaziri wa Kilimo, chakula na ushirika Mhandisi Christopher Chiza

Na Abdulaziz Video,Dodoma
WAKULIMA wa zao la korosho nchini wametakiwa kubadili mitazamo yao kuona zao hilo kuwa la kudumu badala ya kuliona la kujikimu kwa muda na kusababisha kushuka kwa uchumi wao, na kuendelea kuwa masikini, kila mwaka.

Hayo yamebainishwa na waziri wa Kilimo, chakula na ushirika Mhandisi Christopher Chiza wakati alipokuwa anafungua mkutano wa wadau wa korosho wa siku mbili ulifanyika mjini Dodoma.WADAU WA KOROSHOChiza aliyasema hivi sasa za la korosho linazidi kupanuka kiuzalisha
kwa kuongezeka kutoka wilaya 34 hadi 41 na mikoa tisa mipya
inayolima zao hilo Mbeya, Iringa,Njombe, Morogoro,Dodoma Singida.

Alisema kuwa zao hilo bado halijaweza kutoa tija kwa wakulima, kwa
hiyo aliwataka watendaji kutumia vyema kikao hicho kujadili kwa kirefu juu kuleta mabadiliko kwa wakulima na kuondokana na umasikini.

Waziri Chiza alifananisha na mazao mengine ya kudumu kama, Kahawa, migomba ya ndizi, Pamba ambayo yaliweza kuleta sura nzuri ya kiuchumi kwa wakulima wa mazao hayo.WAKUU WA MIKOAHata hivyo aligusia swala zima la ubanguaji wa zao la Korosho, kuwepo na jopo maalumu ambalo litaweza kukaa pamoja na kuhakikisha zao hilo linabanbuliwa nchini. Aliongeza korosho inayosafirishwa ghafi inasababisha hali ya wakulima kuendelea kuwa masikini.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania Anna Abdallah alisema kuwa viwanda bado vinashikiliwa na wafanyabaishara wabangue hapa hapa nchini.WAKUU WA WILAYAAlisema kuwa korosho ghafi soko lake liko sehemu moj tu ni nchini
india jambo linalosababisha kuleta mgongano wa kimaslai kati ya
wanunuzi watendaji wa sekta ya ushirika na walimu.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top