NGOMA AFRICA BAND A.K.A FFU, KUSHEREHEKEA MIAKA 20 YA BAND HIYO

Ngoma Africa Band Live at jambo seehim,Germany  28.07.2013Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" a.k.a FFU yenye makao yake nchini ujerumani. Muzimu huo wa muziki "Ngoma Africa band, utasherekea miaka 20 tangu ianzishwe mwaka 1993 na kiongozi wake  mwanamuziki Ebrahim Makunja almaarufu kamanda Ras Makunja wa FFU.

Bendi hiyo yenye wapenzi,washabiki na wadau lukuki katika kila kona duniani itasherekea miaka 20 ndani ya International African Festival Tubingen 2013,katika viwanja vya Fest-platz huko Tubingen,Ujerumani,ambapo wapenzi wa bendi hiyo wapewa siku mbili kuanzia tarehe 9 na 10.08.2013 kupata burudani ya bendi hiyo.

Ngoma Africa band on stage Jambo seeheim Festiva 2013Ngoma Africa Band a.k.a FFU imetajwa kuwa ndio bendi ya kiafrika hiliyoweza kudumu kwa muda mrefu katika medani ya muziki barani ulaya,na kuweza kujizolea wapenzi na washabiki katika kila kona.

Washabiki na wadau wa bendi hiyo ndio wanao jigamba kuwa wanamiliki na kuipa nguvu bendi hiyo na kiongozi wa bendi hiyo Ras Makunja na wanamuziki wa bendi ni watumishi tu wanao watumikia washabiki na wapenzi wa Ngoma Africa.kamanda ras makunja leader of ngoma africa bandTunaitakia kila la heri Ngoma Africa band tusikose kuwasikiliza FFU at www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-africa.com

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post