Afisa Mfawidhi wa PSPF Mkoa wa Lindi,Delphin Richard akitoa elimu kwa wananchi walojitokeza katika Banda la Mfuko huo katika Maonesho ya Nane nane kanda ya kusini katika Viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi
Bi Olinda Milambo afisa PSPF Makao makuu nae akimuelimisha mteja aliefika katika banda hilo kujua jinsi ya kujipatia nyumba zilizojengwa na PSPF
Na Abdulaziz video,lindiWito umetolewa na Mfuko wa Pensheni kwaWatumishiwaUmma (PSPF)kwa wakazi wa mikoa ya Mtwara na Lindi kujitokeza katika ofisi za mfuko huo zilizo katika mikoa hiyo ili kupata maelezo ya jinsi ya kujiunga mifuko ya Hiari pasipo kuwa Mtumishi wa Umma.
Akiongea na Mtandao katika maonesho ya nne ya Nanenane kanda ya
kusini, Afisa Mfawidhi wa PSPF Mkoa wa Lindi, Delphin Richard ameeleza kuwa mfuko huo kwa kutambua jamii nyingi ambazo hazipo katika Utumishi Ushindwa kumudu maisha kutokana na kutokuwa na uwezo wa kujikimu kunakosababishwa na kutojiwekea akiba na kujua namna ya kukopa na kupata riba anapokuwa na kipato
“Mwandishi PSPF ni Taasisi ya hifadhi ya jamii iliyoanzishwa kwa Sheria Namba 2 ya Mafao ya Hitimisho la Kazi kwa Watumishi wa Umma ya mwaka 1999 (The Public Service Retirement Benefits Act No.2 of 1999) sura ya 371.
Hivyo Hapo awali Mfuko huu ulikuwa unahudumia watumishi wa Serikali Kuu na Wakala wa Serikali tu. Hata hivyo, kufuatia kupitishwa kwa Sheria ya Msimamizi na Mdhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (Sheria Na.8 ya mwaka 2008); fursa zaidi zimefunguliwa ambapo sasa Mfuko wa PSPF unaweza kusajili wanachama kutoka sekta zote iwe sekta binafsi, sekta rasmi na isiyo rasmi”
Aidha mabadiliko haya yameleta uhuru kwa mtumishi kuchagua Mfuko
autakao.Kutokana na hili PSPF inapenda kuwakaribisha wote na inatoa taarifa rasmi kwamba sasa kila Mtanzania aliyekuwepo ndani au nje ya nchi anaweza kuwa mwanachama wa PSPF Ili kuweza kuwahudumia Watanzania wote haswa waliopo katika sekta isiyo rasmi PSPF imeanzisha Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSPF
Supplimentary Scheme) Na Kupitia maonesho haya sasa unaweza kujiwekea akiba kuanzia elfu 10 kwa miezi 12 na unaweza kukopa na kupata Riba sambamba na hilo Zipo Nyumba unaweza kununua kupitia Mafao yako.
Mfuko huo kwa mwaka 2 mfululizo kupitia maonesho hayo ya Nane nane Kanda ya Kusini yanayofanyika katika Viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi ujitokeza ili kusaidia Huduma kwa watumishi na wastaafu ikiwa pamoja na kuhakiki taarifa za wastaafu na Wategemezi
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.