Kijana anayefanya kazi ya ukonda katika daladala inayofanya safari zake kati ya Kitapilimwa - M.R miyomboni Bw Christipher Kinigo akifanya usafi wa kuzoa taka kwa mikono baada ya kunaswa akijisaidia haja ndogo katika eneo hilo kinyume na sheria za usafi Manispaa ya Iringa Hapa akitafakari jinsi ya kuzoa taka kwa mikono baada ya kushindwa kulipa faini ya Tsh 50,000 iliyopangwa na Manispaa ya Iringa kwa wachafuzi wa mazingira Hapa akiwajibika kufanya usafi Hapa koda huyo Bw Christopher anayefanyia kazi katika daladala lenye namba T 228 AMV akizoa taka katika dampo la M.R mchana wa leo Konda huyo akiwa katika daladala analofanyia kazi baada ya kufanya usafi kama adhabu ya kuchafua mazingira.
KONDA wa daladala lenye namba T 228 AMV inayofanya safari zake kati ya Kitapilimwa na M.R- Miyomboni mjini Iringa Bw Christopher Kinigo amepewa adhabu ya kuzoa taka katika dampo kwa mikono baada ya kukutwa akijisaidia haja ndogo kituo cha daladala M.R kando ya barabara ya Mkwawa .
Kijana huyo amekamatwa leo na wadau wa mazingira mjini Iringa ambao wamekuwa wakifanya kazi na mtandao wa matukio daima katika kuweka mji wa Iringa na mkoa wa Iringa katika hali ya usafi.
Hatua ya kijana huyo kufanyishwa usafi imekuja baada ya kuangua kilio akiomba kusamehewa kutokana na kosa hilo na kuwa hakuwa na fedha kiasi cha Tsh 50,000 ambazo ni faini za kisheria kwa wanaokamatwa kwa kuchafua mazingira katika mji wa Iringa.
Akizungumza baada ya kutekeleza zoezi hilo la usafi kijana huyo alisema kuwa ugeni ndio ambao unamsumbua na kuwa anatambua kosa lake na kuwataka vijana wenzake na wananchi wengine kuepuka kuchafua mazingira katika mji wa Iringa.
Kwa mujibu wa mwanasheria wa Manispaa ya Iringa Innocent Kihanga mwananchi atakayekutwa anachafua mazingira kwa kutupa taka ovyo ama kujisaidia maeneo yasiyo rasmi faini yake Tsh 50,000 na mkamataji atalipwa Tsh 20,000 na fedha nyingine zitaingizwa katika mfuko wa usafi wa mazingira mjini Iringa.
Hivyo kuwataka wananchi kuendelea kuwakamata na kuwafikisha ofisi ya manispaa ya Iringa wale wote wanaochafua mazingira ovyo .
Huku mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Terresia Mahongo akipongeza jitihada za wadau wa mazingira mjini Iringa na kutaka kila mwananchi kuhakikisha eneo lake ni safi .
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.