IGP MWEMA AFANYA MABADILIKO YA MAKAMANDA MTWARA NA VIWANJA VYA NDEGE

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
              JESHI LA POLISI TANZANIA

 

Anuani  ya Simu “MKUUPOLISI”                                                             Ofisi ya  Inspekta  Jenerali wa Polisi,
Simu : (022) 2110734                                              Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na. (022)2135556                                                                   S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja:                                                DAR ES SALAAM.

29/08/2013

IGP MWEMA  AWABADILI MAKAMANDA MTWARA NA VIWANJA VYA NDEGE

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema amefanya mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa Mikoa na Vikosi.

Mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara  Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Linus Sinzumwa ambaye amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Idara ya Upelelezi  na nafasi yake inachukuliwa na Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Zelothe Stephen  kutoka Makao Makuu ya Polisi.

Aidha, aliyekuwa Kamanda wa Polisi  Viwanda vya ndege Kamishina Msaidizi (ACP) Deusdedit  Kato amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi  na nafasi hiyo inachukuliwa na Kamishina  Msaidizi wa Polisi (ACP) Selemani Hamisi kutoka Makao Makuu Idara ya Upelelezi.

Wengine ni Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Hamad Hamad anayeenda kuwa Mkuu wa Upelelezi Viwanja vya ndege ambapo hapo awali nafasi hiyo ilikuwa inashikiliwa na David Mwafwimbo aliyehamishiwa mkoani Lindi kuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Lindi (OCD).

Uhamisho huo ni wa kawaida kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.

Imetolewa na:

Advera Senso-SSP

Msemaji wa Jeshi la Polisi.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post